LA LIGA ~ BARCELONA HOI KWA VALENCIA, YAPIGWA 3-2 NYUMBANI.



Mabingwa watetezi wa Ligi kuu nchini Spain Barcelona wamekubali kipigo cha bao 3-2 wakiwa katika uwanja wao wa nyumbani Nou Camp na kuifanya kubaki na pointi zake 54 katika nafasi ya kwanza.

Alexis Sanchez alitangulia kufunga kwa upande wa Barcelona dakika ya 8 tu ya mchezo akipokea pasi murua toka kwa Lionel Messi kabla ya valencia kusawazisha kupitia kwa Daniel Parejo aliyepokea pasi ya Feghouli.

Pablo Piatti aliifungia valencia bao la Pili dakika ya 48 kabla ya Lionel Messi kusawazisha tena kwa njia ya penati hiyo ikiwa ni dakika ya 54.

Valencia walipata bao la Ushindi dakika ya 59 likifungwa na  Francisco Alcacer akipokea pasi toka kwa Feghouli tena bao ambalo liliizamisha kabisa Barcelona na kutoka vichwa chini katika uwanja wao wa nyumbani.

Licha ya Matokeo hayo kutobadili ukweli kwamba Barcelona bado wanaongoza ligi lakini sasa itabidi wasubiri kuangalia matokeo ya Atletico Madrid na Real Madrid ambao wanainyemelea nafasi ya juu katika msimamo.
Hii ni mechi ya Pili msimu huu Barcelona wanapoteza katika Ligi wakiwa wametoka sare 3 na kushinda mechi 17.

Atletico Madrid wana pointi 54 sawa na Barcelona huku Real Madrid wakiwa katika nafasi ya 3 wakiwa na pointi 53.
Atletico Madrdi kesho watacheza na Real Sociedad wakati Real Madrid watacheza na Athletico Bilbao.

+++++++++++++++++++++++++++++++++++++++

No comments

Powered by Blogger.