EPL ~ MAN UNITED YAAMBULIA KICHAPO KINGINE KWA STOKE NI CHA 8 MSIMU HUU
Mabingwa watetezi wa Ligi kuu nchini England Man United leo wamekubali kichapo cha 8 msimu huu baada ya kupigwa bao 2-1 na Stoke City katika mwendelezo wa Ligi kuu nchini England.
Ushindi ambao unaifanya Stoke kushinda kwa mara ya kwanza dhidi ya Man United katika miaka 30.
Man United ikichezesha "Majembe" yake muhimu kama Robin Van Perse,Wayne Rooney na Juan Mata ilishindwa kabisa kupita ukuta wa Stoke City ulioongozwa na Beki wa zamani wa Man United, Showcross na kuambulia goli moja tu lililofungwa na Robin Van Perse huku Charlie Adam akifunga magoli yote ya Stoke City.
Man United ilijikuta ikipoteza wachezaji wawili waliotoka wameumia katika nafasi ya Ulinzi ambao ni John Evans na Phil Jones.
Kwa matokeo hayo Man United inaendelea kubaki katika nafasi ya 7 ikiwa na pointi 40 huku Stoke ikipanda mpaka nafasi ya 11 ikiwa na pointi 25.
MATOKEO MENGINE+++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++
( Borini 19' Johnson 23' Colback 80')
- Newcastle United 0-3 Sunderland
( Kevin Nolan 26',45')
- West Ham 2-0 Swansea
(Snodgrass 5',Bellamy 49' Jones 51')
- Cardiff City 2-1 Norwich City
(Bacuna 34', Naithmith 74',Mirallas 85')
- Everton 2-1 Aston Villa
( Long 12', Paulinho 61')
- Hull City 1-1 Totenham Hotspurs
( Lallana 46',Lambert 70',Rodriguez 75)
- Fulham 0-3 Southampton

No comments