LIGI KUU TANZANIA BARA ~ SIMBA YAUA 4-0 TAIFA. TAMBWE SHUJAA
Mshambuliaji wa Simba Amis Tambwe ameibuka shujaa katika mechi iliyomalizika hivi punde uwanja wa Taifa katika mwendelezo wa Ligi kuu Tanzania Bara baada ya kufunga goli 3 kati ya 4 ambazo Simba ilishinda dhidi ya JKT Oljoro toka Arusha
Tambwe ambaye anaongoza katika orodha ya wafungaji bora wa Ligi kuu baada ya kufunga magoli 13 mpaka sasa alifunga goli 3 katika mchezo huo na kuondoka na mpira wake. Goli lingine la Simba lilifungwa na Jonas Mkude.
Itabidi Simba wajilaumu wenyewe kwa kukosa kutumia nafasi nyingi za wazi na hivyo kushindwa kufunga magoli mengi zaidi.
Kwa Matokeo hayo Simba sasa imefikisha jumla ya pointi 30 katika nafasi ya 4 huku Mbeya City walio na pointi 31 wako katika nafasi ya 3, Yanga wana point 32 katika nafasi ya 2 na Azam FC wakikamata nafasi ya 1 wakiwa na pointi 33.
Kesho Jumapili Yanga wataialika Mbeya City wakati Azam watakua wenyeji wa Kagera Sukari.
+++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++

No comments