LIGI KUU ENGLAND ~ LIVERPOOL YAUA, MAN UNITED YAAMKA HUKU ARSENAL WAKIVUTWA SHATI

Liverpool Imetoa kipigo cha maana kwa Everton kwa kuifunga goli 4-0 katika pambano kali la Ligi kuu England lililopigwa katika uwanja wa Enfield.

magoli ya Liverpool yakifungwa na Steven Gerard dakika ya 21 akipata pasi kutoka kwa Luis Suarez huko goli la pili likifungwa na Daniel Sturridge dakika ya 33 akifunga pia goli la 3 kwa Ufundi mkubwa wa kuwachomoka mabeki waliodhani yuko offside. Goli la 4 likafungwa na Luis Suarez.

Katika mechi Nyingine Vinara wa Ligi hiyo Arsenal waliangukia pua baada ya kukubali sare ya 2-2 na Southampton katika mchezo ulioshuhudia pia mchezaji wa Arsenal Mathew Flamini akipata kadi nyekundu baada ya kucheza rafu.

Magoli ya Arsenal yalifungwa na Giroud na Carzola wakati yale ya Southampton yakifungwa na Jose Miguel Fonte na Adam Lallana.

Kwa Upande wao Mabingwa watetezi Man United wao waliweza kuifunga Cardiff City goli 2-0 Magoli ya United yakifungwa na Robin Van Perse na Ashley Young huku ikishuhudiwa Juan Mata kwa mara ya Kwanza akivaa jezi ya United baada ya Uhamisho wake toka Chelsea.

MATOKEO MENGINE

Norwich 0-0 Newcastle United
Swansea 2-0 Fulham
Crystal Palace 1-0 Hull City

++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++

No comments

Powered by Blogger.