MANCHESTER UNITED HOI LIGI YA MABINGWA. YAPIGWA 2-0 KAMA TIMU ZINGINE ZA EPL
Msimu huu unaendelea kuwa mbaya kwa timu toka ligi kuu England katika hatua hii baada ya timu zake 3 kati ya nne kufungwa bao 2-0 na mechi ambayo wengi walijua ingekua rahisi ni hii ya Manchester United.
Badala yake Man United ilikubali kichapo cha bao 2-0 toka kwa timu ya Olympiacos ya Ugiriki. Man United ikicheza vibaya zaidi na kuwapa wapinzani wao nafasi ya kucheza vile walivyotaka walijikuta wakifungwa bao la kwanza dakika ya 37 Alejandro Dominguez akifunga kwa mpira hafifu na kuifanya timu hiyo kuongoza kwa bao 1-0 mpaka mapumziko
Wengi wakitarajia Man United wangerudi vizuri kipindi cha pili lakini hali ilikua tete zaidi ya kipindi cha kwanza na kujikuta ikipigwa bao la 2 dakika ya 55 kupitia kwa mshambuliaji wa Arsenal aliye kwa mkopo katika klabu ya Olympiacos Joel Campbell na kuzamisha kabisa matumaini ya United kupata japo pointi moja Ugenini.
Mpaka mwisho wa mchezo United ikakubali kipigo cha bao 2-0 hivyo kusubiri mechi ya marudiano mwezi ujao katika Uwanja wa Old Trafford ambapo United itabidi ishinde 3-0 ili isonge mbele.
Katika mechi nyingine ya mapema iliyopigwa Huko Russia ilishuhudiwa Washindi wa pili wa Ligi hiyo mwaka jana Borussia Dortmund walitoa kipigo cha 4-2 kwa wenyeji Zenit.
RATIBA YA LEO
22:45 Galatasaray v Chelsea
22:45 Schalke 04 v Real Madrid
By Edo Daniel Chibo
+++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++

No comments