BARCELONA HALI TETE SPAIN YAKUBALI KICHAPO CHA 3-1 TOKA KWA REAL SOCIEDAD
Mabingwa watetezi Barcelona jana walijikuta wakiangukia "Pua" baada ya kuchapwa bao 3-1 na Real Sociedad katika mchezo mgumu kwa miamba hiyo ya soka duniani.
Kipigo hicho kilikua haki kwa Barcelona ambao walionekana kubanwa sana katika mchezo huo na kama Real Sociedad wangekua makini basi magoli zaidi yangepatikana.
Barcelona walihitaji pointi 3 ili kuweza kuitoa Real Madrid kileleni mwa msimamo wa Ligi baada ya Madrid kushinda 3-0 katika mchezo uliotangulia siku ya jana.
Barcelona ambayo iliwapumzisha baadhi ya nyota wake waliocheza katika mchezo wa ligi ya mabingwa Ulaya dhidi ya Manchester City katikati ya wiki ilitangulia kufungwa goli la kujifunga la dakika ya 32 la Alex Song kabla ya Messi kusawazisha dakika ya 36 na kwenda mapumziko wakiwa sare ya 1-1.
Magoli ya dakika za 54 na 59 ya Grienzmann na Zurutuza yalitosha kuwapa ushindi Real Sociedad ambao hivi sasa wamepanda mpaka nafasi ya 5 wakiwa na point 43 pointi moja nyuma ya nafasi ya kucheza ligi ya Mabingwa Ulaya Msimu ujao.
Kwa Matokeo hayo Barcelona imebaki na point zake 60 katika nafasi ya 2 pointi 3 nyuma ya Real Madrid wanaoongoza Matokeo yanayowafanya walingane kwa pointi na Atletico Madrid ambao wanakamata nafasi ya 3 huku wakiwa na mchezo mmoja mkononi.
Kikosi cha Barcelona kilikua hivi:-
Valdés, Montonya,Adriano,Song,Bartra, Pique,Busquets,Iniesta,Messi,Pedro na Neymar
Real Sociedad Kikosi chao kilikua hivi:-
Bravo,Zaldua,Jose Angel,Elustondo,Gonzalez,Inigo,Zurutuza,Bergara,Vela,Canales na Griezmann
Barcelona sasa imeshindwa kupata ushindi katika uwanja wa Real Sociedad(San Sebastian) katika michezo mitano iliyopita baina ya timu hizo mara ya mwisho Barcelona kushinda hapo ilikua msimu wa mwaka 2006/2007 waliposhinda 2-0 magoli ya Andres Iniesta na Samuel Eto'o.Ligi kuu ya Spain itaendelea leo ambapo Atletico Madrid watakua na nafasi ya kuwaondoa Barcelona katika nafasi ya 2 kama watashinda au kutoka sare watakapocheza na Osasuna katika mchezo utakaopigwa majira ya saa 5 usiku saa za Tanzana.
RATIBA KAMILI - LA LIGA LEO
14:00 Ray Vallecano v SevillaImeandaliwa na Edo Daniel Chibo
19:00 Real Betis v Atletico Bilbao
21:00 Valencia v Granada
23:00 Osasuna v Atletico Madrid
Wapenda Soka - Kandanda
+++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++

No comments