LIGI YA MABINGWA ULAYA~ MAN CITY HOI KWA BARCA WAKATI PSG IKIFANYA KUFURU

Mechi za hatua ya 16 bora ya Ligi ya Mabingwa Ulaya zimeanza kwa Barcelona kuibuka na ushindi wa bao 2-0 wakiwafunga wababe wa Ligi kuu England klabu ya Manchester City katika uwanja wa Etihadi

Magoli ya Lionel Messi na Dan Alves yalitosha kuwapa B
arcelona ushindi muhimu ugenini huku Demicheles wa Man City alipewa kadi nyekundu baada ya kumchezea rafu Messi na Refa akamzawadia kadi nyekundu pamoja na penati ambayo ilifungwa na Messi.

Kwa kifupi mpira ulikua mzuri pande zote wakishambuliana kwa zamu  hata baada ya mchezaji wa City kutolewa japokua Man City sasa watakua na mlima mrefu kuupanda watakaposafiri mpaka Barcelona katika mechi ya Marudiano wiki mbili zijazo ambapo itatakiwa kushinda 3-0 ili kusonga hatua ya Robo fainali.

Katika mechi nyingine PSG wakisafiri mpaka Ujerumani waliweza kuangusha mvua ya mawe baada ya kuwafunga Bayer Leverkusen kwa bao 4-0 magoli ya Matuidi, Ibrahimovic,liyefunga magoli mawil na moja la Yohan Cabaye.

Sasa hali itakua ngumu kwa mabingwa hao wa zamani wa Ulaya Bayer Leverkusenkwani watatakiwa kushinda 5-0 Ufaransa ili waweze kupita raundi hii.

Ligi hiyo itaendelea leo kwa Mechi mbili ambapo Arsenal wataikaribisha klabu bingwa ya Ulaya Bayern Munich pambano litakalopigwa katika uwanja wa Emirates kuanzia saa 4:45 usiku.
Mechi nyingine itakua Ac Milan watakapoikaribisha Atletico Madrid.

+++++++++++++++++++++++++++++++++++++

No comments

Powered by Blogger.