TUZO YA MCHEZAJI BORA WA MWAKA 2013 ~ RONALDO NDO BABA LAO

ASHINDA TUZO KWA MARA YA PILI

Winga mshambuliaji wa timu ya Taifa ya Ureno na klabu ya Real Madrid,Cristiano Ronaldo amechaguliwa kuwa mwanasoka bora wa FIFA wa dunia kwa mwaka 2013 baada ya kuwashinda Lionel Messi wa Barcelona na Timu ya Taifa ya Argentina na Frank Ribery wa Bayern Munich na timu ya Taifa ya Ufaransa.

Hii ni mara ya pili kwa Ronaldo akishinda Tuzo hiyo mara ya kwanza ikiwa ni mwaka 2008 wakati akiichezea Manchester United ya England.

Ronaldo aliyeambatana na mtoto wake na mkewe alijikuta akitoka machozi na kuliza watu wengi alioambatana nao baada tu ya kutangazwa mshindi wa Tuzo hiyo.
Japokua hakushinda kombe lolote akiwa na timu yake ya Taifa wala Klabu ya Real Madrid lakini aliweza kufunga magoli 69 akifunga pia Hat trick mara 8.

Ronaldo ndo mchezaji pekee aliyepiga mashuti mengi katika magoli ya wapinzani kuliko mchezaji yoyote kwa mwaka 2013 huku akitoa pasi za mwisho za magoli 15.
Amekua pia mchezaji wa kwanza katika historia ya Ligi ya mabingwa Ulaya kufunga magoli mengi zaidi katika hatua ya Makundi akifunga magoli 9.
Ronaldo pia amefunga goli 4 katika mechi 2 zilizopelekea timu yake ya taifa ya Ureno kufuzu kwa fainali zijazo za kombe la dunia nchini Brazil dhidi ya Sweden.

Usiku wa jana ulishuhudia pia Tuzo mbali mbali zikitolewa kwa makundi mbali mbali japokua Tuzo ya FIFA fair play ilitia moyo kwa wapenda soka kwani ilinyakuliwa na timu ya Taifa ya Afghanstan mabingwa wa kombe la bara la Asia, ikumbukwe kuwa Afghanstan imekaa zaidi ya miaka 16 bila amani huku Mpira ukirudisha umoja kwa taifa hilo la Asia lililotawaliwa na Vita.

Tuzo zingine zilikua kama ifuatavyo:-

  • Timu bora ya mwaka ya FIFA
  1. Manuel Neur (Germany & Bayern Munich)
  2. Dani Alves (Brazil & Barcelona)
  3. Philip Lahm ( Germany & Bayern Munich)
  4. Thiago Silva ( Brazil & PSG )
  5. Sergio Ramos ( Spain & Real Madrid)
  6. Xavi ( Spain & Barcelona)
  7. Frank Ribery ( France & Bayern Munich)
  8. Iniesta ( Spain & Barcelona)
  9. Zlatan Ibrahimovic ( Sweden & PSG)
  10. Messi ( Argentina & Barcelona)
  11. Ronaldo ( Ureno & Real Madrid)
Huu ni mwaka wa pili sasa ligi inayopendwa Duniani EPL haijawahi kutoa mchezaji katika kikosi hiki na mara ya mwisho ilikua mwaka 2011 wakati Nemanja Vidic na Wayne Rooney walipoingia kutokea Man United ya England.

  • Tuzo ya Heshima ya FIFA
> Jacques Rogge ndo mshindi hapa ambaye amewahi kua mdau mkubwa wa soka hasa upande wa Olimpiki aliwahi kua Raisi wa Kamati ya Olimpiki.
  • Tuzo ya Goli Bora
> Zlatan Ibrahimovic - Goli dhidi ya England
  • Kocha Bora - soka la Wanawake
>  Silvia Neid - kocha wa timu ya taifa ya Ujerumani
  • Kocha Bora - Soka la wanaume
>  Jupp Heynckes - aliyekua kocha wa Bayern Munich.
  • Tuzo Maalumu ya FIFA
>  Pele - Mchezaji wa Zamani wa Brazil
  • Tuzo ya mchezaji bora wa Kike
>  Nadine Angerer (Kipa wa Timu ya Taifa ya Germany)
  • FIFA Ballon d'or
> CRISTIANO RONALDO

++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++

No comments

Powered by Blogger.