BAADA YA TIMU KUBWA ZOTE KUSHINDA SASA LEO ARSENAL NI KUFA AU KUPONA
ILI KURUDI KATIKA NAFASI YA KWANZA INAPASWA KUISHINDA ASTON VILLA LEO..
Pengine leo inaweza kua siku muhimu kwa mustakabali wa Klabu ya Arsenal katika harakati zake za kuwania ubingwa wa Ligi kuu Nchini England watakaposafiri kupambana na Aston Villa walio katika nafasi ya 11 katika msimamo wakati arsenal wao wako katika nafasi ya 3 hivi sasa na ushindi pekee ndiyo utairudisha timu hiyo kileleni Ili kuzitoa Man City na Chelsea pale Kileleni.
Arsenal wanaingia katika mchezo wa leo wakiwa na kumbukumbu mbaya ya kufungwa 3-1 mchezo wa awali ukiwa ni mchezo wa Ufunguzi wa msimu mpya wa Ligi kuu England katika uwanja wa Emirates.
Leo hii Arsenal wataingia katika uwanja wa Villa park wakiwa katika form nzuri sana pengine kuliko miaka 10 iliyopita na lengo kuu leo likiwa ni ushindi.
Katika mechi ya Leo mshambuliaji wa Arsenal Olivier Giroud amerudi kikosini na pengine ataanza leo pia Oxlade- Chamberlain naye akirudi kutoka majeruhi ya muda mrefu. Villa wao kipa Brad Guzan na Mshambuliaji Gabriel Ogbonlahor wakitarajia kuwemo kikosini baada ya kupata majeraha madogo.
Je Villa ataendeleza pale alipoachia mwezi Agosti? Mechi hii itapigwa saa 5 kamili Usiku.
+++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++
Pengine leo inaweza kua siku muhimu kwa mustakabali wa Klabu ya Arsenal katika harakati zake za kuwania ubingwa wa Ligi kuu Nchini England watakaposafiri kupambana na Aston Villa walio katika nafasi ya 11 katika msimamo wakati arsenal wao wako katika nafasi ya 3 hivi sasa na ushindi pekee ndiyo utairudisha timu hiyo kileleni Ili kuzitoa Man City na Chelsea pale Kileleni.
Arsenal wanaingia katika mchezo wa leo wakiwa na kumbukumbu mbaya ya kufungwa 3-1 mchezo wa awali ukiwa ni mchezo wa Ufunguzi wa msimu mpya wa Ligi kuu England katika uwanja wa Emirates.Leo hii Arsenal wataingia katika uwanja wa Villa park wakiwa katika form nzuri sana pengine kuliko miaka 10 iliyopita na lengo kuu leo likiwa ni ushindi.
HISTORIA INASEMAJE?
- Aston Villa haijawahi kuifunga Arsenal wakiwa nyumbani kwao kwa miaka 15 sasa mara ya mwisho kushinda ilikua mwaka 1998 ambapo Villa Ilishinda kwa bao 3-2. Tangu hapo Timu hizo zimekutana mara 14 huku Arsenal wakishinda mara 7 na kutoa sare mara 7
- Katika Mechi 30 kati ya timu hizo katika Ligi baina ya Timu hizo Arsenal wamepoteza mara 3 tu.
- Tangu Ligi ianzishwe mwaka 1992/1993 Aston Villa haijawahi kuifunga Arsenal Nyumbani na ugenini katika msimu mmoja
- Mechi iliyopita katika ligi Aston Villa iliibuka na ushindi wa 1-0 dhidi ya Sunderland na kukomesha ukame wa kucheza mechi 5 mfululizo bila ushindi.
- Villa hawajafunga goli lolote katika mechi Tano kati ya 7 walizocheza nyumbani kwao
- Christian Benteke hajafunga goli lolote katika mechi 11 za ligi mara ya mwisho kufunga ilikua mwezi Septemba dhidi ya Newcastle uNited
- Arsenal imefikisha point 45 baada ya mechi 20 mara ya mwisho kufikisha pointi nyingi hivi baada ya mechi 20 ilikua mwaka 2007/2008 walipofikisha jumla ya point 47.
- Arsenal ndiyo timu pekee katika Ligi kuu msimu huu ambayo imetangulia kufunga goli la kwanza katika mechi nyingi ikitangulia kufunga katika mechi 15 Huku Aston Villa ikiwa ndo timu ya mwisho kutangulia kufunga katika michezo a ligi kuu Ikitangulia kufunga katika mechi 5 tu.
- Mwezi Januari kawaida sio mzuri sana kwa kocha Arsene Wenger kwani katika mechi 9 zilizopita zikichezwa mwezi Januari Arsenal imeshinda mechi 2 tu huku ikitoa sare mechi 2 na kupoteza 5.

No comments