AC MILAN YAMTIMUA KOCHA WAKE
NI MASSIMILIANO ALLEGRI....
Klabu ya AC Milan ya Italia imemtimua kocha mkuu wa Timu hiyo Massimiliano Allegri (Pichani) baada ya mfululizo wa matokeo mabaya ikiwemo kipigo walichokipata jana dhidi ya Sassuolo cha bao 4-3 katika mwendelezo wa ligi kuu nchini Italia maarufu kama Serie A.
Baada ya kipigo hicho AC Milan imejikuta ikikamata nafasi ya 11 katika msimamo wa ligi kuu nchini humo ambapo katika mechi 19 walizocheza wameshinda mechi 5 tu wakatoa sare mechi 7 na kupoteza mechi 7 wakiwa na point 22 pointi 30 nyuma ya Vinara wa ligi hiyo Juventus wenye point 52 wakiwa pia na tofauti ya point 6 tu toka katika mstari wa kushuka daraja.
Katika taarifa kwa vyombo vya habari toka katika timu hiyo ilieleza kua " AC Milan imemfukuza Kocha mkuu Massimiliano Allegri na benchi lake la Ufundi uamuzi ambao unaanza mara moja. AC milan Tunapenda kuwashukuru kocha Allegri na bechi lake la ufundi kwa kazi waliyoifanya na kuwatakia mafanikio mema na kwasasa timu itakua chini ya Kocha msaidizi Mauro Tassotti."
Allegri mwenye umri wa miaka 46 alishatangaza angeiacha Milan baada ya msimu huu kuisha baada ya kujiunga na timu hiyo msimu wa joto mwaka 2010 na kuiongoza Milan kuchukua ubingwa wa Seria A katika msimo huo. Msimu uliofata ilikamata nafasi ya pili wakati msimu uliopita ilikamata nafasi ya 3 baada ya kuuza nyota wake kama Zlatan Ibrahimovic na Thiago Silva walioenda PSG.
Msimu huu Milan Imejikuta ikipigania kutoshuka daraja badala ya ubingwa hali iliyopelekea Bodi kuamua kumtimua kocha huyo ambaye amewahi pia kuzifundisha Aglianese, SPAL, Grosseto, Lecco, Sassuolo na Cagliari.
+++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++
![]() |
| Kocha aliyetimuliwa Allegri |
Baada ya kipigo hicho AC Milan imejikuta ikikamata nafasi ya 11 katika msimamo wa ligi kuu nchini humo ambapo katika mechi 19 walizocheza wameshinda mechi 5 tu wakatoa sare mechi 7 na kupoteza mechi 7 wakiwa na point 22 pointi 30 nyuma ya Vinara wa ligi hiyo Juventus wenye point 52 wakiwa pia na tofauti ya point 6 tu toka katika mstari wa kushuka daraja.Katika taarifa kwa vyombo vya habari toka katika timu hiyo ilieleza kua " AC Milan imemfukuza Kocha mkuu Massimiliano Allegri na benchi lake la Ufundi uamuzi ambao unaanza mara moja. AC milan Tunapenda kuwashukuru kocha Allegri na bechi lake la ufundi kwa kazi waliyoifanya na kuwatakia mafanikio mema na kwasasa timu itakua chini ya Kocha msaidizi Mauro Tassotti."
Allegri mwenye umri wa miaka 46 alishatangaza angeiacha Milan baada ya msimu huu kuisha baada ya kujiunga na timu hiyo msimu wa joto mwaka 2010 na kuiongoza Milan kuchukua ubingwa wa Seria A katika msimo huo. Msimu uliofata ilikamata nafasi ya pili wakati msimu uliopita ilikamata nafasi ya 3 baada ya kuuza nyota wake kama Zlatan Ibrahimovic na Thiago Silva walioenda PSG.Msimu huu Milan Imejikuta ikipigania kutoshuka daraja badala ya ubingwa hali iliyopelekea Bodi kuamua kumtimua kocha huyo ambaye amewahi pia kuzifundisha Aglianese, SPAL, Grosseto, Lecco, Sassuolo na Cagliari.
+++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++

No comments