MAN CITY YAKARIBIA KUMSAJILI "NEYMAR"


Manchester City Inakaribia kukamimilisha usajili kiungo mshabuliaji wa Timu ya taifa ya Nigeria U 17 Musa Yahaya maarufu kama Neymar wa Nigeria.
Yahaya ni kati ya wachezaji walioiongoza Nigeria kutwaa kombe la Dunia la Vijana wa chini ya miaka 17 akifunga goli 4 katika mechi 7 katika michuano hiyo iliyofanyika Falme za Kiarabu mwaka jana huku Nigeria ikiibuka na ushindi wa bao 3-0 dhidi ya Mexico katika mechi ya Fainali na kutwa ubingwa wa Dunia.

Yahaya ambaye amekua akifananishwa sana kiuchezaji na mshambuliaji wa Barcelona na Brazil Neymar amekua akiwindwa pia na Totenham Hotspurs na timu zingine toka Spain na Ureno lakini Man City ndo inayoonekana kufanikiwa katika mbio za kumwania nyota huyo anayechezea Mutunchi Academy ya huko kwao Nigeria.

Yahaya ndoto yake kubwa ilikua kuichezea Real Madrid lakini kwasasa anamwachia meneja wake Babawo Mohammed kushughulikia swala la timu gani aichezee ila kama atasaini kuichezea Man City basi ataungana na mastaa wengine wawili wa Kikosi cha Nigeria U-17 ambao ni straika Kelechi Iheanacho aliyeibuka mfungaji bora wa michuano ya U-17 kwa kufunga magoli 6 na kutengeneza mengine 7 ambaye atasubiri mpaka afikishe miaka 18 ili ajiunge na kikosi hicho cha Manuel Pelegrin.
Mwingine ni Chidi Nwakali ambaye wiki iliyopita alikua Etihadi kukamilisha usajili wake na hii inaonyesha nia ya Man City kuacha matumizi ya pesa nyingi kusajili wachezaji.
+++++++++++++++++++++++++++++++++++++

No comments

Powered by Blogger.