MIWANI PANA YA EDO ~ EUSEBIO 'MWAFRIKA' WA KWANZA KUTIKISA ULIMWENGU WA SOKA



Sanamu ya Eusebio nje ya uwanja wa Benfica
Eusebio da Silva Pereira maarufu kama Eusebio mkali wa kucheka na nyavu aliyejizolea umaarufu mkubwa nchini Ureno hatuko naye tena.
Eusebio Mzaliwa wa msumbiji baba yake akiwa ni raia wa Angola alichukua uraia wa Ureno wakati huo ambao Msumbiji ikiwa ni koloni la Ureno amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 71 akiwa amezaliwa tarehe 25 January 1942.

Eusebio akiwa na Ronaldo
Eusebio katika maisha yake ya soka kwa ngazi ya klabu amecheza timu nyingi ila Benfica ndiyo inabaki kua timu yake itakayomkumbuka milele kwani ameichezea Benfica kwa miaka 15 kati ya miaka 22 aliyocheza soka akichezea michezo 614 na kufunga magoli 638, wastani wa goli moja kila mechi.

Ameshinda mataji 11 ya ligi kuu nchini Ureno na mataji matano ya kombe la Ligi nchini humo, ameisaidia pia Benfica kufika fainali 3 za Ligi ya ubingwa wa Ulaya na kushinda mara moja mwaka 1961-1962.
Amekua pia mfungaji bora wa Ulaya akiwa na Benfica mwaka 1965,1966 na mwaka 1968.
Ameshinda tuzo ya mfungaji bora wa Ligi kuu nchini Ureno maarufu kama Bola De Brata mara 7 ikiwa ni rekodi mpaka sasa.


Katika maisha yake ya Soka Eusebio amecheza mechi 745 katika ngazi ya klabu na kufunga mabao 733 huku akiichezea timu ya taifa ya Ureno kuanzia mwaka
1961 mpaka 1973 na kufunga magoli 41 katika mechi 64.

Katika ardhi ya Ureno anachukuliwa kama ndiyo mchezaji bora zaidi kuwahi kutokea katika nchi hiyo licha ya hivi sasa kuibuka Cristiano Ronaldo kwani ndiye aliyeiongoza Ureno kushika nafasi ya tatu katika fainali ya Kombe la Dunia mwaka 1966 akiwa mfungaji bora wa michuano hiyo akifunga goli 9 zikiwemo goli 4 alizofunga katika mechi moja dhidi ya timu ya Taifa ya Korea Kaskazini.

Eusebio amewahi kushinda pia tuzo ya mwanasoka bora wa Dunia maarufu kama Ballon d'or mwaka 1965 akiwa ndo mtu wa kwanza mwenye ngozi nyeusi kushinda kama sijakosea.
Pia amekua mshindi namba mbili wa tuzo hizo mwaka 1962 na 1966.


Mpaka umauti unamkuta Eusebio amekua balozi wa mpira wa miguu akihamasisha mchezo huo duniani.


+++++++++REST IN PEACE LEGEND++++++

....Imetayarishwa na
Edo Daniel Chibo (facebook)

No comments

Powered by Blogger.