BAADA YA ARSENAL KUTANGULIA JANA LEO KIBARUA KIKO KWA MAN UNITED WAKATI CHELSEA NA LIVERPOOL WAKIPATA MITEREMKO


Raundi ya tatu ya Kombe la chama cha soka Nchini England ilianza jana ambapo michezo kadhaa ikipigwa huku Matokeo ya kushangaza yakiwa Man City kutoka sare ya 1-1 na Blackburn Rovers na Aston Villa wakitupwa nje ya mashindano hayo kwa kufungwa na Sheffield United  2-1.

Blackburn Rovers inayoshiriki ligi daraja la kwanza sasa wanapata nafasi ya kurudiana na Man City katika mechi ya marudiano itakayopigwa katika dimba gumu la Etihad nyumbani kwa Manchester City.

Arsenal wao walikua na mzigo mkubwa kuutua pale walipowakaribisha majirani zao Totenham Hotspurs katika mchezo mwingine wa michuano hiyo uliopigwa katika dimba la Emirates ambapo Arsenal walio katika fomu hivi sasa waliwafunga Spurs bao 2-0 magoli ya Santiago Carzola na Tomas Rosicky.

Cardiff City ikiwa na kocha wao mpya Ole Gunnar Solskjaer waliifunga Newcastle bao 2-1 ugenini magoli ya Cardiff yakifungwa na Craig Noone na Fraizer Campbell huku Newcastle wakitangulia kufunga kwa goli la Papis Cisse.
Ilikua mara nyingine kwa Ole Gunnar Solskjaer kubadilisha matokeo kama alivyokua akizoeleka pale alipokua akiichezea Man United na kubatizwa jina la "Super Sub" kwani Newcastle walikua mbelea kwa bao 1 kabla ya mchezo kubadilika baada ya mabadiliko yaliyofanywa na Ole hatimaye kurudisha na kuongeza goli.

Timu nyingine zinazoshiriki ligi kuu ya England matokeo yake yalikua kama Ifuatavyo
Crystal Palace waliifunga West Brom goli 2-0 huku Southampton wakifunga Burley goli 4-3, Everton wakaifunga QPR goli 4-0.
Wakati Mabingwa Watetezi wa kombe hilo Wigan walilazimishwa sare ya 3-3 na M.K. Dons.

Mechi za Kombe hilo zitaendelea leo ambapo Ratiba inaonyesha itakua vita nyingine ya kupata matokeo kwa kocha wa Man United David Moyes pale watakapoikaribisha Swansea katika dimba la Old Trafford mahali ambapo pamezalisha matokeo mabaya kwa United msimu huu.

Chelsea wao wamepata mteremko watakaposafiri kuikabili Derby inayofundishwa na kocha wa zamani wa England Steve McLaren wakati Liverpool watakua nyumbani kuwaalika Oldham inayoshiriki ligi daraja la pili nchini England

Ratiba kamili iko kama Ifuatavyo:-
  • 15:00  Nottm Forest v West Ham
  • 17:00  Sunderland v Carlisle
  • 17:05  Derby v Chelsea
  • 18:00  Liverpool v Oldham
  • 18:00  Port Vale v Plymouth
  • 19:30  Man United v Swansea
Zingatia: muda huu ni kwa masaa ya Afrika Mashariki.
 
 

No comments

Powered by Blogger.