LIGI KUU ENGLAND ~ MAN UNITED YAANZA MWAKA VIBAYA
![]() |
| Adebayor akifunga goli la kwanza |
Mabingwa watetezi wa ligi kuu Nchini England Manchester United wamejikuta wakianza mwaka vibaya baada ya kukubali kichapo cha bao 2-1 toka kwa Totenham Hotspurs nyumbani.
Hii ni mara ya pili mfululizo kwa Totenham kuibuka na ushindi katika Uwanja wa Old Trafford kwani mara ya mwisho iliibuka na ushindi wa 3-2 msimu uliopita wakati kocha Alex Ferguson akiendelea kuifundisha Man United kabla ya hapo Spurs ilikua haijawahi kushinda katika uwanja huo kwa miaka 23.
![]() |
| Eriksen akifunga goli la pili |
Spurs walipata magoli yao kupitia kwa Emmanuel Adebayor na Christian Eriksen huku lile la United likifungwa na Danny Welbeck.
Huu ni ushindi mzuri kwa Kocha mpya wa timu hiyo Tim Sherwood kwani katika michezo minne iliyopita hajawahi kupoteza mchezo wowote.
Kwa upande wao United kipigo hicho kinakomesha ushindi wa mechi 6 mfululizo katika mashindano yote na kuifanya kuwa nyuma kwa tofauti ya point 11 na anayeongoza Ligi Arsenal.
Hii ni mechi ya kwanza kwa timu hizo katika raundi ya pili ya ligi kuu nchini England.
Matokeo mengine katika mechi za mwaka mpya yalikua hivi:-
- Swansea 2-3 Man United
- Arsenal 2-0 Cardiff City
- Crystal Palace 1-1 Norwich
- Fulham 2-1 West Ham
- Liverpool 2-0 Hull City
- Southampton 0-3 Chelsea
- Stoke 1-1 Everton
- Sunderland 0-1 aston Villa
- West Brom 1-0 Newcastle United


No comments