LIGI KUU ENGLAND ~ LIVERPOOL YASIMAMISHWA HUKU MAN CITY IKIENDELEZA UBABE


Ligi kuu ya England imeingia patamu baada ya Man City kushinda 2-1 dhidi ya liverpool. Magoli ya Man City yakifungwa na Nahodha Vicent Kompany na Alvaro Negredo katika mchezo ulioonekana kuwa wa kasi tangu dakika ya kwanza mpaka dakika ya mwisho.

Kwa Ushindi huo Man City Inapanda mpaka nafsi ya pili ikiwa na pointi 38 yani pointi 1 tu nyuma ya Arsenal wanaoongoza na hii inaifanya Liverpool kushuka mpaka nafasi ya 4 katika Msimamo.

Manchester City inaendelea kuwa mbabe katika michezo yote iliyopigwa katika uwanja wao Wa nyumbani katika ligi kuu kwani mpaka sasa haijapoteza mchezo wowote katika mechi zote zilizochezwa katika uwanja wa Etihad

Arsenal wanaongoza wakiwa na pointi 39, Man City wako nafasi ya pili wakiwa na pointi 38
Chelsea iko katika nafasi ya Tatu ikiwa na pointi 37 huku Liverpool ikikamilisha 4 bora.

No comments

Powered by Blogger.