ZAWADI ZA BOXING DAY ~ ARSENAL YARUDI KILELENI, SPURS YABANWA WAKATI EVERTON IKIANGUKIA PUA
Arsenal imewapa zawadi ya Krismasi mashabiki wake baada ya kuchomoa goli 1 na kushinda 3-1 dhidi ya West Ham magoli mawili ya Theo Walcot na moja la Lucas Podoski huku West Ham wakitangulia kufunga kupitia kwa Carton Cole dakika ya 47.
Kwa matokeo hayo Arsenal Inapanda mpaka nafasi ya kwanza kileleni ikiwa na point 39 ikifatiwa na Chelsea yenye point 37 baada ya kupata ushindi wa goli 1-0 dhidi ya Swansea goli la Eden Hazard.
Timu zilizo katika hatari ya kushuka daraja, Sunderland na Crystal Palace leo zimejikongoja na kuongeza pointi baada ya kushinda mechi zao za leo.
Sunderland ikiifunga Everton bao 1-0 goli la penati dakika ya 25 la kiungo wa Swansea anayecheza kwa mkopo katika timu hiyo Ki Sung-Yueng.
Crystal Palace wao kwa upande wao wameishinda Aston Villa bao 1-0 goli la dakika ya 90 la Dwight Gayle.Totenham baada ya kuonja ushindi katika mechi iliyopita leo imevutwa shati na West Brom baada ya kulazimishwa sare ya 1-1 Spurs wakitangulia kufunga kwa goli la Christian Eriksen dakika ya 36 kabla ya Jonas Olsson kusawazisha dakika mbili baadae.
Matokeo mengine yameshuhudia Southampton ikiifunga Cardiff City goli 3-0 magoli ya Jay Rodriguez dakika ya 14 na 20 na Rickie Lambert dakika ya 27.
Newcastle ikaifunga Stoke City 5-1 magoli ya Loic Remy dakika 44 na 56, Yoan Gouffran dakika ya 48,Yohan Cabaye dakika ya 66 naPapiss Cisse dakika ya 80.
Goli Stoke lilifungwa na Oussama Asaidi.
Mchezo mmoja umebaki kati ya Manchester City na Liverpool Je Liverpool atarudi kileleni?
>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>><<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<

No comments