BOXING DAY ~ MAN UNITED YATOA ZAWADI KWA MASHABIKI WAKE .



Manchester United imewapa zawadi ya Krismas mashabiki wake baada ya kurudisha magoli mawili na kuongeza moja hatimaye kuibuka na ushindi wa goli 3-2 dhidi ya Hull City katika uwanja wa Kingston Communication nyumbani kwa Hull City.

Hull city walianza mchezo kwa kasi na kupata magoli mawili yaliyosababishwa na uzembe wa Mabeki wa United kupitia kwa James Chester dakika ya 4 na lingine likifungwa na David Meyler dakika ya 13.

Chriss Smalling alifunga goli la kwanza la United dakika ya 19 akiunganisha mpira wa adhabu uliopigwa na Wayne Rooney. Dakika ya 26 Man United ilipata goli la kusawazisha baada ya Wayne Rooney kupiga shuti la umbali wa karibia mita 25 na kumshinda kipa Adrian wa Hull City. James Chester wa Hull City alijifunga akiwa katika harakati za kuokoa mpira wa krosi ya Ashley Young dakika ya 66 na kuiandikia United bao la ushindi.

Huu ni ushindi wa Tano mfululizo kwa kocha David Moyes na kuifanya kufikisha michezo 9 ugenini bila kufungwa  katika mashindano yote mara ya mwisho kufungwa ugenini msimu huu ilikua dhidi ya Manchester City.

Kwa matokeo hayo Man United imefikisha pointi 31 katika nafasi ya 6 hii ni kabla ya michezo ya Totenham wanaocheza dhidi ya West Brom na ule wa Newcastle na Stoke City.

Katika mechi hiyo Rafael alitoka kwa upande United baada ya kuumia nafasi yake ikachukuliwa na Adnan Yanuzaj na Antonia valencia alitolewa baada ya kupewa kadi mbili za njano

>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>><<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<

No comments

Powered by Blogger.