MIWANI PANA YA EDO ~ MECHI 5 ZINAZOWEZA KUBADILI MWELEKEO KATIKA LIGI KUU ENGLAND MSIMU HUU
Ligi kuu nchini England imeingia patamu sana baada ya timu 8 zote kuwa na nafasi ya kuchukua ubingwa zikiwa zimebaki mechi 2 mzunguko wa kwanza kumalizika.
Tofauti kati ya anayeongoza ambaye ni Liverpool na anayekamata nafasi ya 8 (Man United) ni point 8.
Hapa ndipo Miwani yangu pana ilipoamua kuangazia mechi 5 zinazofata kwa kila timu baada ya Chistmas ili kujua kama nafasi zitabaki kama zilivyo au zitapanguka kutokana na matokeo.
Baada ya Christmas ni Boxing Day na hapa utaziweza kuziona klabu zote zikicheza katika mwendelezo wa ligi hiyo.
Zifuatazo ni timu 8 bora kwasasa katika ligi na mechi zao 5 zinazoikabili kila moja
Baada ya ukame wa muda mrefu Liverpool wamerudi katika chati na hadhi yake kwani mpaka Christmas wanaongoza ligi hii ni mara ya kwanza huku Suarez akiongoza pia katika upachikaji mabao.
Liverpool ndo timu pekee iliyofunga magoli mengi msimu huu nyuma ya Manchester City ikiwa imeshafunga magoli 42 ikiwa na pointi 36.
Je hizi juhudi zilizoonyeshwa na Liverpool msimu huu zitadumu mpaka mwisho na kuja kuchukua ubingwa wa England baada ya miaka zaidi ya 20?
Hebu tuangalie sasa mechi 5 zinazoikabili Liverpool katika ndoto zake za kuchukua ubingwa msimu huu.
Arsene Wenger anaiongoza Arsenal katika msimu wa 9 bila kikombe chochote na jinsi msimu ulivyoanza ni dhahiri mashabiki wa Arsenal wanategemea kitu msimu huu na kwa hali ilivyo ni kuchukua ubingwa wa England ndicho wanachotarajia mashabiki hasa baada ya kukaa kileleni muda mrefu.
Arsenal ndo timu pekee katika historia ya ligi kuu nchini England kumaliza ligi bila kufungwa mchezo wowote lakini kwa muda mrefu imekaa bila kuonja utamu wa kubeba ubingwa wa ligi hiyo.
Wakiwa wameongoza ligi kwa kipindi kirefu msimu huu wanakamata nafasi ya 2 nyuma ya Liverpool wakilingana kwa pointi 36.
Ili Arsenal wachukue ubingwa wanatakiwa kupata matokeo mazuri kwanza katika mechi Tano zinazoikabili hivi sasa ambazo ni:-
Timu pekee ambayo watu wengi wanaipa nafasi ya kuchukua ubingwa msimu huu ni Manchester City ambayo inakamata nafasi ya 3 ikiwa na point 35 lakini imefunga magoli 51 mpaka sasa hii inakuonyesha jamaa hawana mchezo katika kufunga na hii ndo timu pekee ambayo haijapoteza mchezo katika uwanja wake wa nyumbani.
Ndiyo timu pekee iliyochukua point nyingi kwa timu ambazo ni vigogo wa ligi hiyo ila mechi 5 zijazo zinaweza kuamua mustakabali wa timu hiyo katika mbio zake za kubeba ubingwa mechi hizo ni:-
Kwa mara ya pili sasa Kocha Jose Mourinho anaifundisha Chelsea lakini mara hii mambo yamekua magumu kwake kwani mpaka sasa Chelsea inakamata nafasi ya 4 ikiwa na point 34 sawa na Everton inayokamata nafasi ya 5.
Zifuatazo ni mechi ambazo pengine zinaweza kuipeleka Chelsea Juu au kuishusha:
Baada ya Kocha David Moyes na Kiungo Marouane Fellaini kutimkia Man United Everton imeweza kusimama na kupigana kiume chini ya kocha Roberto Martinez kwani mpaka sasa inakamata nafasi ya 5 nyuma ya Chelsea wote wakiwa na pointi 34.
Mwanzo umekua mzuri kwao ila michezo mitano ijayo inaweza kuamua hatma ya timu hiyo na michezo hiyo ni:-
Hii ndo timu inayozidi kushangaza wengi huku ikiwa na wachezaji wengi Wafaransa Newcastle imefanikiwa kumaliza nafasi ya 6 tangu ligi ianze mpaka kufikia Christmas huku ikipata pointi muhimu toka kwa Chelsea,Man United na Spurs.
Ina kibarua kigumu kuhakikisha haiporomoki hapo ilipo kwani ina pointi 30 hivi sasa sawa na Totenham iliyo katika nafasi ya 7 na hizi ndo mechi 5 ambazo pengine zikaamua mustakabali wa timu hiyo.
Baada ya kumtimua kocha Totenham imeanza kurudi mchezoni huku ikiwapa nafasi wachezaji ambao walikua hawapati nafasi kama Emmanuel Adebayor.
Adebayor amefunga magoli matatu katika mechi mbili mpaka sasa tangu aondoke kocha AVB.
Inakamata nafasi ya 7 ikiwa sawa na Newcastle kwa pointi 30 kila moja pointi 6 nyuma ya Vinara Liverpool. Ikiwa imetumia pesa nyingi kusajili wachezaji msimu huu ni dhahiri lengo lake ni kumaliza ikiwa ndani ya timu nne bora ili ikacheze ligi ya mabingwa Ulaya mwakani, Ina mtihani mkubwa kufikia mafanikio hayo kwani imezungukwa na timu kubwa zinazowania nafasi nne za juu pia.
Mechi 5 zinazoikabili Spurs ni pamoja na :-
Mabingwa watetezi wa Ligi kuu nchini England wanakamata nafasi ya 8 katika msimamo wa ligi msimu huu. Baada ya Sir Ferguson kutangaza kustaafu na David Moyes kuchukua mikoba yake timu imepitia mengi ikiwa ni pamoja na kufungwa na timu ndogo ikiwa katika uwanja wake wa nyumbani.
Hii ndo timu ya mwisho kwa upande wangu ambayo kama itachanga karata zake vizuri inaweza kuibuka na Ubingwa kwani imepitwa point 8 na wanaoongoza Ligi. Michezo mitano ijayo inaweza kuamua ni nini Man United itavuna msimu huu michezo hiyo ni pamoja na:-
>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>........>>>>>>
Until Next time................
Edo Daniel Chibo (Facebook)
mfalme.edo@gmail.com (email)

- LIVERPOOL

- Manchester City vs Liverpool (Ugenini)
- Chelsea vs Liverpool (Ugenini)
- Liverpool vs Hull City (Nyumbani)
- Stoke City vs Liverpool (Ugenini)
- Liverpool vs Aston Villa (Nyumbani)
- ARSENAL
Arsene Wenger anaiongoza Arsenal katika msimu wa 9 bila kikombe chochote na jinsi msimu ulivyoanza ni dhahiri mashabiki wa Arsenal wanategemea kitu msimu huu na kwa hali ilivyo ni kuchukua ubingwa wa England ndicho wanachotarajia mashabiki hasa baada ya kukaa kileleni muda mrefu.
Arsenal ndo timu pekee katika historia ya ligi kuu nchini England kumaliza ligi bila kufungwa mchezo wowote lakini kwa muda mrefu imekaa bila kuonja utamu wa kubeba ubingwa wa ligi hiyo.
Wakiwa wameongoza ligi kwa kipindi kirefu msimu huu wanakamata nafasi ya 2 nyuma ya Liverpool wakilingana kwa pointi 36.
Ili Arsenal wachukue ubingwa wanatakiwa kupata matokeo mazuri kwanza katika mechi Tano zinazoikabili hivi sasa ambazo ni:-
- West Ham vs Arsenal (Ugenini)
- Newcastle vs Arsenal ( Ugenini)
- Arsenal vs Cardiff City (Nyumbani)
- Aston Villa vs Arsenal (Ugenini)
- Arsenal vs Fulham (Nyumbani)
- MANCHESTER CITY
Timu pekee ambayo watu wengi wanaipa nafasi ya kuchukua ubingwa msimu huu ni Manchester City ambayo inakamata nafasi ya 3 ikiwa na point 35 lakini imefunga magoli 51 mpaka sasa hii inakuonyesha jamaa hawana mchezo katika kufunga na hii ndo timu pekee ambayo haijapoteza mchezo katika uwanja wake wa nyumbani.
Ndiyo timu pekee iliyochukua point nyingi kwa timu ambazo ni vigogo wa ligi hiyo ila mechi 5 zijazo zinaweza kuamua mustakabali wa timu hiyo katika mbio zake za kubeba ubingwa mechi hizo ni:-
- Man City vs Liverpool (Nyumbani)
- Man City vs Crystal Palace (nyumbani)
- Swansea vs Man City (Ugenini)
- Newcastle vs Man City ( Ugenini)
- Man City vs Cardiff City
- CHELSEA
Kwa mara ya pili sasa Kocha Jose Mourinho anaifundisha Chelsea lakini mara hii mambo yamekua magumu kwake kwani mpaka sasa Chelsea inakamata nafasi ya 4 ikiwa na point 34 sawa na Everton inayokamata nafasi ya 5.
Zifuatazo ni mechi ambazo pengine zinaweza kuipeleka Chelsea Juu au kuishusha:
- Chelsea vs Swansea (Nyumbani)
- Chelsea vs Liverpool ( Nyumbani)
- Southampton vs Chelsea (Ugenini)
- Hull City vs Chelsea (Ugenini)
- Chelsea vs Man United (Nyumbani)
- EVERTON
Baada ya Kocha David Moyes na Kiungo Marouane Fellaini kutimkia Man United Everton imeweza kusimama na kupigana kiume chini ya kocha Roberto Martinez kwani mpaka sasa inakamata nafasi ya 5 nyuma ya Chelsea wote wakiwa na pointi 34.
Mwanzo umekua mzuri kwao ila michezo mitano ijayo inaweza kuamua hatma ya timu hiyo na michezo hiyo ni:-
- Everton vs Sunderland (Nyumbani)
- Everton vs Southampton (Nyumbani)
- Stoke vs Everton (Ugenini)
- Everton vs Norwich (Nyumbani)
- West Brom vs Everton (Ugenini)
- NEWCASTLE UNITED
Hii ndo timu inayozidi kushangaza wengi huku ikiwa na wachezaji wengi Wafaransa Newcastle imefanikiwa kumaliza nafasi ya 6 tangu ligi ianze mpaka kufikia Christmas huku ikipata pointi muhimu toka kwa Chelsea,Man United na Spurs.
Ina kibarua kigumu kuhakikisha haiporomoki hapo ilipo kwani ina pointi 30 hivi sasa sawa na Totenham iliyo katika nafasi ya 7 na hizi ndo mechi 5 ambazo pengine zikaamua mustakabali wa timu hiyo.
- Newcastle vs Stoke (Nyumbani)
- Newcastle vs Arsenal (Nyumbani)
- West Brom vs Newcastle ( Ugenini)
- Newcastle vs Man City ( Nyumbani)
- West Ham vs Newcastle ( Ugenini)
- TOTENHAM HOTSPURS
Baada ya kumtimua kocha Totenham imeanza kurudi mchezoni huku ikiwapa nafasi wachezaji ambao walikua hawapati nafasi kama Emmanuel Adebayor.
Adebayor amefunga magoli matatu katika mechi mbili mpaka sasa tangu aondoke kocha AVB.
Inakamata nafasi ya 7 ikiwa sawa na Newcastle kwa pointi 30 kila moja pointi 6 nyuma ya Vinara Liverpool. Ikiwa imetumia pesa nyingi kusajili wachezaji msimu huu ni dhahiri lengo lake ni kumaliza ikiwa ndani ya timu nne bora ili ikacheze ligi ya mabingwa Ulaya mwakani, Ina mtihani mkubwa kufikia mafanikio hayo kwani imezungukwa na timu kubwa zinazowania nafasi nne za juu pia.
Mechi 5 zinazoikabili Spurs ni pamoja na :-
- Totenham vs West Brom (nyumbani)
- Totenham vs Stoke City (Nyumbani)
- Man United vs Totenham (Ugenini)
- Totenham vs Crystal Palace (Nyumbani)
- Swansea vs Totenham (Nyumbani)
- MANCHESTER UNITED
Mabingwa watetezi wa Ligi kuu nchini England wanakamata nafasi ya 8 katika msimamo wa ligi msimu huu. Baada ya Sir Ferguson kutangaza kustaafu na David Moyes kuchukua mikoba yake timu imepitia mengi ikiwa ni pamoja na kufungwa na timu ndogo ikiwa katika uwanja wake wa nyumbani.
Hii ndo timu ya mwisho kwa upande wangu ambayo kama itachanga karata zake vizuri inaweza kuibuka na Ubingwa kwani imepitwa point 8 na wanaoongoza Ligi. Michezo mitano ijayo inaweza kuamua ni nini Man United itavuna msimu huu michezo hiyo ni pamoja na:-
- Hull City vs Man United (Ugenini)
- Norwich vs Man United ( Ugenini)
- Man United vs Totenham (Nyumbani)
- Man United vs Swansea (Nyumbani)
- Chelsea vs Man United ( Ugenini)

No comments