CAPITAL ONE ~ MAN UNITED KUSUKA AU KUNYOA LEO

Mechi za nusu fainali ya kombe la Ligi nchini England maarufu kama Capital One zinaanza kupigwa usiku huu kwa Sunderland kuwakaribisha mabingwa Watetezi wa Ligi kuu Manchester United huku mechi ya marudiano ikipigwa baada ya wiki mbili katika uwanja wa Old Trafford.
Adnan Januzaj alifunga goli 2 mara ya mwisho zilipokutana hizi timu

Sunderland inakamata nafasi ya Mwisho katika msimamo wa Ligi kuu huku Man United wao wakiwa katika nafasi ya 7 mpaka sasa.
Timu zote hizi zilikua katika mechi za Kombe la FA mwishoni mwa wiki iliyopita ambapo United walitupwa nje ya michuano hiyo kwa kufungwa goli 2-1 na Swansea wakati Sunderland wao waliitupa nje Timu ya Carlisle kwa kuifunga 2-0.

Pengine huu unaweza kuwa msimu mbaya zaidi kwa Man United hasa kwa Matokeo katika Ligi huku kombe hili likiwa ni mojawapo ya kombe ambalo kidogo wana uhakika nalo wakati Sunderland watakua wakijifariji hasa kwakua katika nafasi ya kushuka daraja mpaka sasa hali kama hii ilizikuta pia Birmigham City na Wigan misimu ambayo timu hizo zilishuka daraja.

HISTORIA INASEMAJE KUHUSU TIMU HIZO?
  • Katika Michezo 20 kati ya timu hizo Sunderland haijawahi kushinda mchezo wowote mpaka sasa katika mashindano yote.
  • Mara Ya mwisho United kufungwa na Sunderland ilikua katika muda wa nyongeza mwaka 2000 goli 2-1  katika mashindano ya kombe la ligi.
  • Sunderland imefika fainali mara moja tu ya kombe hilo la Ligi mwaka 1985 ikipoteza kwa bao 1-0 dhidi ya Norwich City katika uwanja wa Wembley
  • Sunderland ambayo inanolewa na Gus Poyet imeshinda mechi zake zote tano katika kombe la Ligi na Kombe la FA msimu huu.
  • Man United haijafungwa goli lolote katika mechi tatu za michuano hiyo ikizitoa timu zote zinazoshiriki ligi kuu ambazo ilipangwa nazo ambazo ni Liverpool,Stoke na Norwich.
  • Katika mechi 7 za ugenini Man United haijawahi kufungwa huku ikishinda mechi 3 mfululizo zilizopita
  • Chicharito amefunga magoli matano msimu huu, matatu kati ya hayo akiyafunga katika kombe la ligi (Capital One)
...... Note: Mechi Hii inaanza saa 4:45 Usiku huu katika Uwanja wa Mwangaza nyumbani kwa Sunderland.

              +++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++++

No comments

Powered by Blogger.