KOMBE LA LIGI ~ UNITED HALI MBAYA, YAPOTEZA MICHEZO YOTE TANGU MWAKA UANZE



Hali imezidi kua mbaya kwa Kikosi cha kocha David Moyes baada ya kuambulia kichapo cha bao 2-1 toka kwa Sunderland mchezo uliopigwa katika dimba la Mwangaza na kuifanya ipoteze michezo yote mitatu kwa mwaka huu.

Goli la kwanza la Sunderland lilifungwa na beki wa Zamani wa Man United Phil Basley baada ya Ryan Giggs kushindwa kuokoa mpira wa krosi uliopigwa kutoka pembeni hivyo kufanya mpaka mapumziko ubao kuonekana ni 1-0

Kipindi cha Pili United walikuja na kasi na kufanya mashambulizi ya mara kwa mara hatimaye kupata goli kupitia nahodha wake Nemanja Vidic akiunganisha mpira wa kona ya Tom Cleverley

Goli la pili la Sunderland lilifungwa na Fabio Borini kwa penati baada ya Adam Johnson kuangushwa ndani ya eneo la hatari.

Mechi ya marudiano itapigwa Old Trafford baada ya wiki mbili.

No comments

Powered by Blogger.