MIWANI PANA YA EDO ~ CHELSEA vs MAN UNITED, NI KAMA MECHI YA MTANI JEMBE BONGO

Mwezi uliopita kulikua na pambano la kirafiki la watani wa jadi katika soka la Tanzania kati ya Simba na Yanga huku Simba ambayo ilikua dhoofu ilhali ikiibuka na Ushindi wa bao 3-1 katika pambano ambalo kila mtu alitegemea Simba atafungwa goli nyingi sana. Hapa ndipo napata kuamini kama soka ni dakika 90 uwanjani na sio maneno ya nje ya uwanja.

Leo katika jiji la London Nchini England litapigwa pambano la ligi kuu nchini humo kati ya Mabingwa watetezi Manchester United ambao wako na Msimu mbaya watakapoikabili timu inayopewa nafasi ya kuchukua ubingwa msimu huu Chelsea iliyo chini ya kocha Jose Mourinho.

NI VITA KATI YA MOURINHO v MAN UNITED

Man United ndo mabingwa wa kihistoria wa soka la England wakichukua ubingwa wa Ligi kuu mara 20 na miaka yote hiyo imekua na rekodi nzuri ya kuzinyanyasa karibia timu zote England isipokua Chelsea na hasa Chelsea inayonolewa na Kocha Jose Mourinho.

Mourinho ndo kocha pekee aliyeweza kuisumbua United kwa miaka yote kwani katika mara 17 ambazo amekutana na United ni mara mbili tu amepoteza na hii ni tangu akiwa FC Porto,Chelsea na Real Madrid swali hapa litakua je Vita hii stering atauawa kama muvi za kihindi au ataendeleza Ubabe kama Steven Seagal?

Pia Jose Mourinho anatafuta ushindi wake wa 100 tangu aanze kuifundisha Chelsea katika Ligi kuu nchini England.

Ukiangalia kwa makini msimu huu Tangu Mourinho arudi Chelsea mipango yake mingi ni kupata walau pointi 4 kwa timu zile kubwa yani sare ugenini na ushindi nyumbani na amefanikiwa kwa hilo kwani ametoka sare na Man United katika Mechi ya kwanza pale Old Trafford kisha akatoa sare na Arsenal pale Emirates wakati alishatoka sare na Spurs wakiwa 10 uwanjani  huku akizifunga Man City na Liverpool darajani.

UHALISIA UKOJE MPAKA SASA.
Hii ni mechi ambayo Man United wanatakiwa kushinda kwa namna yoyote japokua Mourinho hajawahi kufungwa pale darajani. Kama United itashinda basi itaongeza matumaini kwa mashabiki juu ya Uwezo wa kocha David Moyes na kama watafungwa basi watakua pointi 12 nyuma ya Chelsea na point 14 nyuma ya Arsenal wanaoongoza.

Man United imeshinda mechi 5 kati ya 4 zilizopita katika ligi kuu msimu huu na njia pekee ya kurudi katika mstari ni kuanza na ushindi dhidi ya Chelsea je litawezekana hilo?

HISTORIA

  • Man United imeshinda mechi nyingi katika uwanja wa Stamford Bridge kuliko Chelsea,Ikishinda mechi 30 huku Chelsea ikishinda 22.
  • Mechi ya mwisho kukutana timu hizo Hapo Darajani Man United iliibuka kidedea kwa kuifunga Chelsea bao 3-2.
  • Katika Mechi 6 zilizopita katika ligi Chelsea imeshinda 5 na kutoka sare 1 huku ikiruhusu goli 2 tu.
  • Huu ni mchezo wa 19 tangu Chelsea Kufungwa mara ya Mwisho hapo Darajani tangu walipofungwa na QPR Januari 2,2013
  • Danny Welbeck amefunga magoli katika mechi 3 zilizopita za Ligi na ndo mshambuliaji atakayeongoza mashambulizi leo dhidi Chelsea.
Naishia hapa kwa sasa ila nabaki kujiuliza je Yanaweza kutokea yale ya mtani jembe?


........ Unaweza kuwasiliana nami kupitia
>  Edo Daniel Chibo (Facebook)
>  EdoDanielChibo ( Instagram)
>  EdoDaniel1 (twitter)
> Email mfalme.edo@gmail.com

No comments

Powered by Blogger.