LIGI KUU ENGLAND ~ BINGWA MTETEZI MAN UNITED YAPIGWA TATU NA CHELSEA

SASA NI NDOTO KUTETEA UBINGWA

Mabingwa watetezi wa ligi kuu England Man United imekubali kipigo cha 3-1 toka kwa Chelsea katika uwanja wa Stamford bridge maarufu kama Darajani. Samuel Etoo akiibuka shujaa baada ya kufunga magoli yote matatu.
Goli la Kufutia machozi la United lilifungwa na Javier Hernandez Chicharito aliyeingia kipindi cha pili akichukua nafasi ya Ashley Young.

Japokua United waliongoza kwa umiliki wa mpira lakini walishindwa kabisa kutoka na magoli katika pambano hilo huku safu yake ya Ulinzi ikionyesha udhaifu mkubwa huku Chelsea wakiwa na safu bora ya Ulinzi na kuwazuia kabisa wachezaji wa United.

Kwa matokeo hayo Man United inaendelea kubaki katika nafasi ya 7 ikiwa na pointi 37 huku Chelsea wakipanda mpaka nafasi ya 3 wakiwa na point 49 pointi 2 nyuma ya Arsenal wanaoongoza ligi.

Katika Mechi hiyo Nahodha wa United Nemanja Vidic alitolewa nje kwa kadi nyekundu baada ya kumchezea vibaya Edin Hazard ambapo sasa ataikosa mechi dhidi ya Sunderland katika kombe la Ligi na mechi dhidi ya Cardiff City zote hizi zikipigwa katika dimba la Old Trafford.

Katika mechi ya awali leo Spurs waliifunga Swansea bao 3-1 magoli mawili ya Emmanuel Adebayor na goli la kujifunga la Chico Flores huku Swansea wakipata goli lao kupitia kwa Bonny.

++++++++++++++++++++++++++++++++++

No comments

Powered by Blogger.