WAKATI AVB AKITIMULIWA,ZOLA AOMBA KUACHIA NGAZI
AVB |
Ule msemo wa makocha wanaajiriwa ili kufukuzwa Umeendelea tena mwishoni mwa wiki baada ya aliyekua kocha wa Totenham Hotspurs Andre Villas Boas kutimuliwa katika nafasi hiyo aliyodumu nayo kwa miaka miwili sasa na hii imekuja baada ya kukubali kichapo cha mabao 5-0 nyumbani toka Kwa Liverpool katika Ligi.
Kipigo hicho hakijawahi kutokea kwa Timu hiyo inayotokea London kwa zaidi ya miaka 16 sasa. AVB amejiunga na Spurs miaka miwili iliyopita baada ya kutimuliwa Chelsea
Spurs inakamata nafasi ya 7 katika msimamo wa ligi kuu England wakiwa na point 27 baada ya michezo 16.
Japokua inasuasua katika Ligi lakini Spurs inafanya vizuri katika mechi za kimataifa hasa kombe la Europa kwani imeshinda mechi zote 6 ilizocheza na kufikisha pointi 18.
Kwa upande mwingine pia aliyekua kocha wa Watford Giafranco Zola naye amebwaga manyanga baada ya kushuhudia timu yake ikifanya vibaya zaidi tangu kuanza kwa msimu huu tofauti na ilivyokua msimu uliopita ambapo aliweza kuiongoza Watford mpaka hatua ya mtoano ya kutafuta nafasi ya kucheza ligi kuu.
Watford imeshindwa kupata ushindi Katika mechi 9 zilizopita kwa kupoteza michezo yote ndani yake wakipoteza mara 5 mfululizo na inakamata nafasi ya 13 katika msimamo wa ligi ya Championship.
No comments