LIGI YA MABINGWA ULAYA ~ MAN UNITED YAPIGA 5 HUKU PUNGUFU MADRID WAKIIZODOA GALA MARA 4
Mabingwa wa England Man United wametinga hatua ya 16 bora kwa staili ya namna yake baada ya kuibuka na ushindi wa bao 5-0 ugenini wakiifunga Bayer Leverkusen.
Man United iliingia katika mchezo huo ikiongoza kundi A kwa pointi 8 wakifatiwa na Leverkusen wenye pointi 7 hivyo kikosi cha David Moyes kilihitaji ushindi tu ili kujihakikishia nafasi ya kucheza hatua inayofata.
Antonio Valencia alifungua ukurasa wa magoli kabla ya Emir Spahic kujifunga na kwenda mapumziko United wakiongoza 2-0. Kipipindi cha Pili United waliongeza magoli matatu kupitia kwa John Evans,Criss Smalling na luis Nani.
Mechi nyingine ya kundi hilo Ilishuhudia Shaktar Donesk ikiifunga Real Sociedad goli 4-0 na kuifanya kufikisha pointi 8 ikishika nafasi ya 2 nyuma ya Man United yenye pointi 11 ambayo pia ishafuzu baada za michezo ya leo.
Mechi za mwisho za kundi hili Man united wataikaribisha Shaktar wakati Leverkusen watasafiri kuikabili Real Sociedad.
Katika Kundi B Real Madrid wakicheza pungufu baada ya Ramos kupata kadi nyekundu walibamiza Galatasaray inayofundishwa na kocha wa zamani wa Man City Roberto Mancin goli 4-1 ukiwa ni mchezo wa 38 mfululizo Madrid wanafunga goli katika ligi ya Mabingwa Ulaya.
Magoli ya Madrid yakifungwa na Gareth Bale,Arbeloa, Di Maria na Isco wakati lile la Galatasaray lilifungwa na Umut Balut.
Mechi nyingine ya kundi hilo ilishuhudia Juventus wakiibuka na ushindi wa 3-1 dhidi ya FC Kobenhavn magoli yote ya Juventus yakifungwa na Artudo Vidal mawili yakiwa ya Penati.
Kwa matokeo hayo Real Madrid wanaendelea kuongoza wakiwa na point 13 huku Juventus wakiwa na point 6 wakati Galatasaray na Kobenhavn wakiwa na point 4 hivyo kufanya mechi za mwisho kuvutia sana.
Katika kundi C PSG wakiwa tayari wameshavuka waliwakaribisha Olympiacos na matokeo ni kwa PSG kushinda 2-1 magoli ya Ibrahimovic na Cavan.
Katika mechi nyingine ya kundi hilo Benfica ikiwa Ugenini iliweza kuibuka na ushindi wa 3-2 dhidi ya Anderlecht.
Kwa Matokeo hayo PSG wanaongoza wakiwa na point 13 wakati Olympiacos na Benfica wakiwa na pointi 7 huku Anderlecht wakikamata mkia na pointi yao 1.
Kundi D ilikua ni vita ya kupigania kuongoza kundi hilo kati ya mabingwa Watetezi Bayern Munich na Man City kwani baada ya mechi za leo bayern Munich wanaendelea kuongoza wakiwa na pointi 15 huku Man City wakiwa na pointi 12 huku mechi ya mwisho itakua kati ya wababe hao wawili.
Bayern Munich ilipata ushindi wa 3-1 dhidi ya CSKA Moscow huku Man City ikishinda 4-2 Nyumbani dhidi ya Viktoria Plzen.
Kabla ya usiku huu mechi kadhaa zilipigwa siku ya Jumanne na kwa kifupi matokeo yalikua hivi:-
Zenit 1-1 Atletico Madrid
Fc Basel 1-0 Chelsea
Steau 0-0 Schalke 04
Arsenal 2-0 Marseille
Dortmund 3-1 Napoli
Fc Porto 1-1 Austria Vienna
Ajax 2-1 Barcelona
Celtic 0-3 AC Milan
No comments