MIWANI PANA YA EDO ~ WAKALI WATANO BORA WALIOFANYA VIZURI WIKIEND HII KATIKA EPL


Weekend imeisha kwa michezo mingi kupigwa katika ligi kuu nchini England magoli mengi yakipatikana
MIWANI YANGU PANA imeniongoza kusema mechi kati ya Everton na Liverpool ndiyo mechi bora kabisa kwa weekend hii ikitawaliwa na ujanja wa hali ya juu, Ufundi na kila aina ya raha ya mpira huku magoli 6 yakifungwa katika sare ya 3-3 katika uwanja wa Goodson Park.

Wikiendi imeshuhudia Arsenal wakijiimarisha katika nafasi ya kwanza kwa kuifunga Southampton 2-0 nyumbani sifa zimwendee Olivier Giroud aliyepiga magoli yote mawili

Najaribu kuvua miwani sasa ili niweze kuandika nilichokiona katika mechi kadhaa na hapa nawaangazia wale wakali Watano ambao wametia fora hasa kwa michango yao uwanjani:-

  • FRAIZER CAMPBELL - CARDIFF CITY

Mshambuliaji wa zamani wa Man United na Sunderland anaichezea Cardiff City kwasasa alikua mwiba mchungu kwa timu yake ya zamani Man United katika sare ya
2-2 katika uwanja wa Cardiff huku akifunga goli la kwanza na kusumbua vilivyo ngome ya United mpaka alipotolewa kipindi cha pili huyu nampa namba Tano katika orodha yangu
Ka kasi ambayo Campel aliionyesha ni dhahiri kijana anawania nafasi ya kucheza timu ya Taifa ya England.
  • SIMON MIGNOLET - LIVERPOOL
 
 
Kama Liverpool watamaliza Top 4 basi ni dhahiri mchango wa kipa huyu raia wa Ubelgiji  hautasahaulika kwani Kwa mara nyingine ameonyesha kua Brendan Rodgers hakukosea kumsajili toka Sunderland.
Mignolet alikua mhimili mkubwa wa kuzuia mashuti ya washambuliji wa Everton ni kipa aliyeonekana kujiamini muda wote wa mchezo uyu nampa nafasi ya 4 kwani japokua alifungwa goli 3 lakini aliweza kuoko nyingi za wazi.
 
 
  • JONJO SHELVEY - SWANSEA CITY

Wakiwa Ugenini Swansea City waliweza kupata ushindi wa 2-1 dhidi ya Fulham huku kiungo wa timu hiyo Jonjo Shelvey akiwika vilivyo na kuwa sababishi ya ushindi wa Swansea ambao umeifanya kuingia katika timu 10 bora katika msimamo kwasasa
Huyu nampa namba namba 3 katika orodha ya wachezaji waliofanya vizuri wikiendi hii.
  •  FRANK LAMPARD - CHELSEA

Frank Lampard kwa mara nyingine alirudi Upton Park mahali alipoanzia soka na kufunga magoli mawili kati ya matatu ambayo Chelsea walikua wamepata.
Lampard anaendelea kufunga na kuizidi rekodi ya muda mrefu iliyowekwa na gwiji wa Chelsea Bobby Tambling
Licha ya miaka mingi aliyonayo katika soka lakini Lampard amezidi kuonekana ni bora kadri muda unavyoenda ni kati ya wachezaji wachache ambao viwango vyao katika soka vimeendelea kuwa juu
 Nampa nafasi ya Pili katika orodha ya wachezaji waliofanya vizuri wikiendi iliyopita
 
 
  • SERGIO KUN AGUERO - MAN CITY

Sergio Aguero mpaka sasa amefunga magoli 20 katika mechi 20 alizocheza msimu huu akiwa na Man City. Segio alifunga magoli mawili katika ushindi wa 6-0 ambao City wameupata dhidi ya Totenham Hotspours.
Namba moja imeenda kwa huyu jamaa kwa kuendeleza kiwango bora msimu huu na kumweka kati ya washambuliaji wakali kabisa duniani kwasasa.
Mchango wa Aguero ulikua mkubwa sana katika mechi hiyo na nimeweza kuishuhudia City ikicheza mpira kwa umakini mkubwa kutoa pasi nzuri na kujiwekwa sehemu nzuri ya kuweza kufunga.


Kwa haraka miwani yangu pana kabisa iliweza kuyapata haya tu tukutane wakati wengine tukiangalia kitu kingine.
 
 
~ Edo Daniel Chibo ~

No comments

Powered by Blogger.