THE GUNNING MACHINE ~ JE SILAHA ZINATOSHA KUBEBA UBINGWA KATIKA MSITU WA MAADUI WENYE UCHU?



Baada ya kipindi kirefu kutokua hewani sasa makala yako mahususi kwa ajili ya yanayoihusu klabu ya Arsenal (The gunners) Imerudi tena na leo tutaangalia Je Silaha zetu ghalani zitatosha kubeba ubingwa katika msitu wa maadui waliokamilika?

Kwanza mpaka Ninaandika makala hii Arsenal ndo inayoongoza ligi kuu nchini England baada ya michezo 11 safari ikipitia vikwazo vingi kila mmoja akiamini jeshi litashindwa mwezi huu mara mwezi ujao lakini hali ikawa nyofu mpaka sasa mwezi wa 11 huku Jeshi likitoa makamanda Wawili Yani mchezaji bora wa mwezi mara moja na kocha bora wa mwezi mara moja huu ni mwanzo mzuri kabisa katika kuelekea kuwa bingwa mpya wa msimu huu baada ya kukaa na ukame muda mrefu.

Arsenal leo tuko Nyumbani kuikaribisha timu inayoshika nafasi ya tatu ya Southampton na ushindi pekee leo ndiyo utaendeleza uhakiki wa kushinda vita hii. Southampton si timu ya kuidharau kwani inaingia leo ikiwa na Rekodi ya kupata matokeo mazuri ugenini dhidi ya Liverpool na Manchester United na pia haijafungwa katika mechi 8 zilizopita.

Kwakifupi kuhusu mechi hiyo ni kwamba Per  Mertesacker atarudi baada ya kuikosa mechi dhidi ya Man United ugenini lakini Flamini bado yuko nje. Mara ya mwisho Southampton kuja Emirates tuliwafunga 6-1 Septemba mwaka 2012 japokua timu inayokuja leo ni tofauti na ile ya mwaka jana.

Mara ya mwisho Arsenal kufungwa nyumbani na Southampton ilikua mwaka 1987 goli la Danny Wallace na Ushindi leo utaifanya Arsenal kushinda mechi ya tano mfululizo katika ligi wakiwa nyumbani mara ya mwisho kufanya hivyo ilikua April Mwaka jana.
Mechi iliyopita dhidi ya Man Unted ndo mechi pekee ambayo Arsenal imeshindwa kufunga goli lolote katika ligi mara ya mwisho kufanya hivyo ikiwa ni  April 16 mwaka huu Tulipotoka sare na Everton.

Sasa leo sitaki kuiangalia sana mechi hii mana ubingwa hauchukuliwi kwa ushindi wa mechi moja tu ila nataka kuangalia ukubwa na uwezo wa jeshi pamoja na silaha zetu zitatusaidiaje kubeba ubingwa katika lundo la maandui msimu huu.

Taarifa zilizopo ni kwamba Theo Walcot anarejea katika kikosi baada ya kumkosa kwa mechi kadhaa huku kukiwa na imani Lucas Podoski na Chemberlain wako mbioni kurudi hizi ni taarifa nzuri kwani kila mmoja anafahamu umuhimu wa Theo kikosini japokua ujio wake pia unaweza ukamfanya Wenger asisajili na kuridhika.

Je Jeshi linatosha?

Ukiangalia kwa upana wa jeshi letu utagundua safu ya ushambuliaji hasa wamaliziaji hakuna hapo ndo ninapozielewa zile tetesi za kuwahusisha wachezaji kama Luis Suarez, Fernando Loriente na Wayne Rooney kuhamia Emirates kwani mpaka sasa uwiano wa magoli uko hivi: Jumla ya magoli 22 yamefungwa na Arsenal msimu huu lakini ni goli 5 pekee zimefungwa na Washambuliaji wakati Viungo wamefunga magoli 15 na mabeki goli 2.

Ukiangalia hapo kwa haraka au hata kwa makini utagundua Jeshi linakosa wamaliziaji hii inawafanya viungo kutafuta nafasi za kufunga badala ya kutengeneza nafasi za washambuliaji kufunga.

Najaribu kuangalia Mabingwa waliopita wa ligi kuu England Msimu uliopita Man United wakati wanachukua ubingwa walikua na Robin Van Perse ambaye amebobea katika kufunga huku wanaomsaidia wakiwa wengi kama Rooney,Welbeck na Chicharito  lakini kwa upande wetu Tulikua na Olivier Giroud na bado tunaye huyo huyo wa kiwango cha juu japo yupo Bendtner lakini si mchezaji wa kumtegemea kwa timu kubwa kama Arsenal na hapo  ndo naomba na kusali Wenger anunue mshambuliaji wa maana ili kumaliza vita hii mapema.

Zipo timu ambazo ziliwahi kutegemea Viungo na zikaweza kufanikiwa je sisi tutaweza kufanikiwa kwa kutegemea Viungo pekee? Kwangu mimi jibu ni hapana bado anahitajika mtu atakayemsaidia Giroud kufunga, Bado mtu anahitajika atakayezigeuza zile pasi za Mesut Ozil kuwa magoli na kuhakikisha ushindi kila mechi. bado anahitajika mtu atakayetengeneza nafasi ili Ramsey asiwaze sana kufunga bali kumwekea.

Msimu huu Arsenal tumeonekana kuimarika na ushindi umekua ukipatikana na hii ndiyo yaniaminisha kuwa Jeshi litamaliza katika mstari wa mbele tofauti na msimu uliopita kwani kwa msimu uliopita baada ya mechi 11 Arsenal ilikua katika nafasi ya 5 ikiwa na point 16 tu huku Man Utd waliokuja kuwa mabingwa wakikamata nafasi ya kwanza wakiwa na point 27, Man City nafasi ya pili wakiwa na point 25, Chelsea nafasi ya tatu wakiwa na pointi 24, Everton ikikamata nafasi ya 4 wakiwa na point 20.(Hiyo ni kwa mechi 11 za mwanzo tu)

 Lakini msimu huu mambo ni tofauti kabisa kwani Arsenal tuko juu baada ya mechi hizo 11 ila sisi tuna point 25 tukifatiwa na Liverpool wenye point 23, Southampton inakamata nafasi ya 3 ikiwa na pointi 22, Chelsea ikiwa katika nafasi ya 4 na point zake 21 huku Man United ikishika nafsi ya 5 na point zake 20.

Bado nina Matumaini na Jeshi letu likiongozwa na na kocha mzoefu Arsene Wenger ila inatubidi kuangalia hii vita tunayopigana tuna maadui gani hivyo wamaliziaji wanahitajika kutuimarisha zaidi

.... Go gunners

.>>>> Imendaliwa na Mdau wa Arsenal Kijiji cha Makumbusho

No comments

Powered by Blogger.