CRISTIANO RONALDO ANATOKEA SAYARI NYINGINE - ANCELOTT


Kocha mkuu wa Timu ya Real Madrid ya Hispania Carlo Ancelott amefunguka na kumwagia sifa Winga mshambuliaji wa timu hiyo, Mchezaji wa Zamani wa Dunia na nahodha wa timu ya Taifa ya Ureno Cristiano Ronaldo kama Mchezaji toka Sayari nyingine.

Ancelott ametanabaisha kua kwa jinsi Ronaldo anavyofunga inashangaza na inamtenga na wachezaji wengine na kumweka katika kundi tofauti kabisa inayopelekea kuonekana kama anatoka Sayari nyingine nje ya Dunia.

Juzi Cristiano Ronaldo alifunga goli muhimu kwa timu yake ya Taifa ya Ureno walipoikaribisha Sweden na pengine goli hilo likawapeleka katika Fainali za kombe la Dunia Nchini Brazil mwakani.
Mechi ya Marudiano itapigwa nchini Sweden Jumanne ya Wiki hii ambapo macho yatakua yakiwaangazia Cristiano Ronaldo na Zlatan Ibrahimovic wa Sweden ambaye juzi hakuwika huku Ureno wakihitaji Sare tu katika mechi ya marudiano ili kupata nafasi

Real Madrid iko katika Nafasi ya Tatu katika msimamo wa ligi kuu nchini Spain ikiwa na pointi 31 ikiongozwa na mabingwa Watetezi Barcelona wenye point 37 wakifatiwa na Mabingwa wa Kombe la Mfalme Atletico Madrid wenye point 34 huku kila timu ikiwa imeshacheza michezo 13.

Ronaldo mwenye miaka 28 alifunga Hat-trick (magoli matatu) yake ya 23 na ya 19 katika La Liga wiki iliyopita katika ushindi wa bao 5-1 walioupata Real Madrid dhidi ya Real Sociedad na hii ni tangu alipojiunga na Real Madrid mwaka 2009 akitokea Man United.

Amekua msaada mkubwa sana kwa klabu yake na hapo ndipo unapoweza kuamini usemi wa Ancelott kuwa jamaa ni spesho kwani katika mechi 3 zilizopita Real Madrid wameweza kufunga jumla ya magoli 15 huku magoli 8 kati ya hayo yakifungwa na Ronaldo.
Tangu msimu huu uanze Ronaldo amefunga magoli 28 katika mechi 20 alizocheza kwa Klabu yake na timu ya Taifa ya Ureno na katika hayo ana hat trick 4.

Ronaldo amefunga magoli 225 katika mechi 216 ambazo ameichezea Real Madrid katika mashindano yote pamoja na mechi za kirafiki lakini pia amefunga magoli 162 katika mechi 148.

Watu wengi Tunaamini kuwa huu ni mwaka wake Ronaldo kubeba tena tuzo ya mwanasoka bora wa Dunia  na hata kocha wake Ancelott anaamini hivyo ila Swali ni je Ataweza kupata kura nyingi safari hii kumzidi Lionell Messi ambaye ameshinda tuzo hiyo kwa mara 4 mfululizo?

No comments

Powered by Blogger.