NIGERIA NA IVORY COAST WATANGULIA BRAZIL KUPITIA AFRIKA
Nigeria ilikua nyumbani kuwakaribisha Ethiopia na ikaweza kuibuka na ushindi wa 2-0 magoli ya Victor Moses na Victor Obinna. Ushindi ambao umeifanya nigeria kupata tiketi ya kucheza fainali hizo kwa jumla ya magoli 4-1 baada ya kupata ushindi wa 2-1 jijini Adis Ababa Ethiopia.
Kwingineko wababe wa soka la Afrika Ivory Coast wakiwa na Nyota wao kibao kama Didier Drogba, Kalou,Gervinho, Yaya na Kolo Toure walikua na wakati mgumu kuwakabili Simba wa milima ya Terranga Timu ya Taifa ya Senegal na kadri muda ulivyosogea ndipo hali ilipokua ngumu kwa miamba hao wa Afrika kwani ni dhahiri walionekana kuzidiwa.
Goli la dakika ya 77 la mshambuliaji wa Senegal aliyeingia kipindi cha pili Moussa Sow liliamsha matumaini ya Senegal kufuzu kwani walihitaji goli moja zaidi ili wapate nafasi
Ivory Coast ambao waliingia katika mchezo huo wa pili kucheza na Senegal walikua na faida ya ushindi wa 3-1 walioupata katika mechi ya kwanza jijini Abdijan.
Solomon Kalou akaifungia Ivory Coast goli muhimu dakika ya 3 ya muda wa nyongeza ikihakikisha nafasi ya Ivory Cost katika fainali hizo na kufanya mchezo huo kumalizika kwa sare ya 1-1 hivyo Ivory Coast kupita kwa jumla ya magoli 4-2.
Nigeria na Ivory Coast wataungana na washindi watatu wa mechi zilizobaki kwa kanda ya Afrika kutimiza nafasi 5 ambazo Afrika wamekua nazo katika uwakilishi.
'''''''''''''''''''''''''''''''''''''''''
Sijaona mpambanaji halisi kati ya timu hzi mbili zilizofuzu! Mpambanaji aliye tayari kutetea nchi yake hatoki Nigeria au Ivory Coast bhana!
ReplyDeleteEdo umepotea sana kwenye hii blogu man! Nikakuwait Man U vs Arsenal lakini wapi
Daaaah kuna mabo yalikua yamenibana sana ila sasa nimerudi tegemeeni mengi kutoka hapa
DeleteKuhusu hawa wawakilishi wa Afrika kwa mtazamo wangu mimi zingeenda timu za Waarabu ndo tungefika mbali hawa mabrazameni wa West Africa hawana jipya Mpira mbovu kabisa wa Ivory Coast wakicheza na Senegal mpaka naanza kuamini kama hawa Jamaa huwa wanatumia Ndumba (am jst saying)
Leo ni Tunia vs Cameroon ningefurahi hapa kama Tunisia angepita
....Edo