LIGI YA MABINGWA ULAYA ~ ARSENAL YAHARIBU "BESIDEI" YA WENGER


Usiku ambao Kocha wa Arsenal Arsene Wenger alikua akisherekea kutimiza miaka 64 ya kuzaliwa uliharibiwa na kipigo walichopata Arsenal toka kwa Borussia Dortmund toka Ujerumani katika ligi ya mabingwa Barani Ulaya.

Goli la kustukiza la Dortmund dakika ya 16 likiwekwa kimiani na Henrik Mkhitaryan akipata pasi toka Kwa Lewandowski liliwaamsha Arsenal na kushambulia kwa umakini mkubwa na kufanikiwa kupata goli dakika ya 41 likifungwa na Olivier Giroud.

Roberto Lewandowski alikamilisha ushindi wa Dortmund kwa kufunga bao safi dakika ya 82  na kupoteza matumaini kabisa ya Arsenal kuongoza kundi hilo.
Kwa matokeo hayo Kundi hilo linazidi kua gumu kwani Timu tatu zina Point 6 ambazo ni Arsenal,Napoli na Dortmund huku Marseille  wakitoka patupu mpaka sasa.

Katika mechi nyingine za Ligi ya Mabingwa Ulaya Chelsea waliishushia kipigo kikali cha 3-0 Schalke 04 ya Ujerumani Magoli mawili ya Fernando Torres na Eden Hazard

Barcelona wakisafiri mpaka Jiji la Milan walilazimisha sare ya 1-1 Milan wakitangulia kufunga kupitia kwa Robinho kabla ya Messi kuisawazishia Barcelona.

Zenit kutoka Russia walisafiri kuwakabili FC Porto ya Ureno na Zenit kuibuka na ushindi wa bao 1-0 goli la Alexandr Kerzhakov.

Napoli ikisafiri mpaka Ufaransa ilijinyakulia point tatu muhimu wakishinda 2-1 magoli ya Calejon na Zapata huku lile la Marseille likifungwa na Andre Ayew.

Steau Bucaresti wakiwa nyumbani walilazimisha sare ya 1-1 na FC BASEL.

No comments

Powered by Blogger.