MECHI YA WATANI WA JADI ~ SIMBA YAWEKA HISTORIA TAIFA
... YACHOMOA BAO 3 NA KULAZIMISHA SARE NA YANGA
Pengine leo yaweza kua siku nyingine baada ya kipigo cha 5-0 mwaka Jana siku ambazo mashabiki wa Yanga hawataamini kilichotokea uwanjani.
Wachambuzi wengi wa Soka leo waliipa nafasi yanga kufanya vizuri uchambuzi ambao ulionekana kuwa sahihi baada ya Yanga kupata magoli matatu ya haraka kipindi cha kwanza na kuwafanya kwenda mapumziko wakiwa mbele kwa magoli hayo matatu ambayo yalifungwa na Mrisho Khalfan Ngassa na Hamis Kiiza ambaye alifunga magoli mawili.
Mpaka mapumziko mashabiki walio na mioyo myepesi wa Simba waliamua kuondoka uwanjani hasa baada ya kuona hakuna dalili ya magoli kurudi ila ilikuwepo dalili ya magoli kuongezeka.
Katika kipindi hicho cha kwanza Yanga waliweza kumiliki mpira jinsi walivyotaka huku Simba wakionekana kupoteana kabisa huku Yanga wakimiliki mpira kwa asilimia 52 Simba wao walikua na umiliki wa asilimia 48
yanga wakipiga mashuti matano golini huku Simba wakipiga mashuti manne yaliyolenga goli.
Kipindi cha Pili Simba walionekana kubadilika na mabadiliko yaliyofanywa ya kumtoa Chanongo na kuingia Ndemla yalileta Uhai na simba kuweka historia ambayo haijawahi kuwekwa baina ya timu hizo kwani waliweza kurudisha magoli mawili ya haraka kupitia kwa Betram Mwombeki aliyepiga shuti kali ndani ya 18 huku Joseph Owino akifunga kwa kichwa akiunganisha mpira wa kona.
Zikiwa zimebaki dakika chache mpira kumalizika wengi tuliamini matokeo yatabaki 3-2 lakini Gilbert Kaze beki huyu wa Simba raia wa Burundi alifunga bao safi akiunganisha mpira wa adhabu uliopigwa na nahodha wa Simba Chollo na kufanya Dakika 90 kumalizika kwa sare ya 3-3.
Kwa matokeo ya leo sasa Simba wanabaki katika nafasi ya 3 wakiwa na pointi 19 nyuma ya Azam na Mbeya City huku Yanga wakibaki katika nafasi ya 5 wakiwa na pointi 16.

No comments