MIWANI PANA YA EDO ~ SABABU 5 ZA KUAMINI KWANINI YANGA ILIFUNGWA NA SIMBA KATIKA MECHI YA NANI MTANI JEMBE




Nani mtani Jembe? nadhani baada ya tambo na majigambo ya zaidi ya mwezi mmoja sasa hatimaye imejulikana kuwa Simba ndiyo mtani jembe baada ya kushinda mechi yake dhidi ya Yanga kwa jumla ya goli 3-1.

Viunga vingi vya jiji la Dar Es Salaam jana vilipambwa na bendera nyingi za timu hizo hasa zaidi Yanga ambao walikua wakiongoza katika kukusanya pesa katika shindano lililochezeshwa na Wadhamini bia ya Kilimanjaro kabla ya mchezo uliopigwa Uwanja wa Taifa.

Jambo kubwa lililosababisha Yanga kufungwa ni kuzidiwa kimchezo japokua miwani yangu pana iliweza kuangalia mambo mengine matano ambayo pengine yalisababisha Yanga kupoteza mchezo huo

· Kujiamini kupita kiasi kwa wachezaji,mashabiki na hata viongozi.

Ligi kuu Tanzania bara imesimama kwasasa mpaka tarehe 25 huku Yanga wakiongoza na Simba wako katika nafasi ya 4 na Yanga wakionekana kufanya vizuri sana katika mzunguko wa kwanza huku Simba wakimaliza mzunguko wa kwanza kwa kusuasua. Kisha Simba wakaingia katika mgogoro mkubwa uliopelekea kutimuliwa kwa makocha wa timu hiyo. Siku chache kabla ya mechi ya Mtani Jembe Yanga wakamsajili aliyekua mshambuliaji wa Simba Emmanuel Okwi na kutangaza kama atacheza katika mchezo huo.

Matukio yote hayo yanaweza kukuonyesha kwa jinsi gani Yanga walivyokua wamejiamini hii iliwapa mwanya wa kubweteka kama wangeshinda goli nyingi tu wakati Simba wao njia pekee kwao kupunguza migogoro ilikua ni kushinda hivyo basi timu iliandaliwa mahususi kwa ushindi huku uzoefu wa kocha msaidizi Selemani Matola ambaye amekaa amekaa muda mrefu na kikosi cha vijana wa Simba ambao wengi wako kikosi cha wakubwa sasa kama Singano, Mkude n.k

· Umri wa Wachezaji

Ukiangalia kwa haraka kikosi cha Yanga kimesheheni wachezaji wengi ambao umri wao ni mkubwa kiuhalisia tofauti na Simba ambao wametumia vijana wengi ambao ndo kwanza wanaanza kuchipukia katika soka.

Hii inawapa faida Simba kwani Vijana hao wengi wanatafuta mafanikio lakini kwa Upande wa Yanga wachezaji wengi wameshafikia kikomo angalia mchezaji kama Juma Kaseja,Ngassa n.k hawa wameshawika sana nchi hii na hapo ndipo naamini kama umri wao pia umeshasogea.



· Kuwa na wachezaji wengi waliokua wakicheza Simba

Hii sababu inaweza kuonekana ni ya kijinga ila ina maana sana ukiiangalia kwa undani swala hili utagundua kama uwepo wa wachezaji wengi ambao walishaichezea Simba unawafanya wachezaji hao kucheza kwa uoga hasa kwa kukumbuka yaliyomtokea kipa wa Timu hiyo Barthez siku Yanga walipotoka sare ya 3-3 na Simba katika ligi.


Hapo ndipo utakubaliana nami baada ya makosa aliyoyafanya Juma Kaseja jana na kupelekea Simba kushinda goli la 3 lakini kwa upande wa Simba wao hawana kitu hicho wachezaji walijiamini na kufata vyema maelekezo ya kocha.

· Ushindi wa Goli 5 ambazo Simba iliwahi kuwafunga Yanga

Kila mara zinapotokea mechi za Simba na Yanga wazo kubwa wanaloingia nalo Yanga uwanjani ni kulipiza kisasi cha magoli yale 5-0 ambayo Simba waliyapata wakiifunga Yanga. Simba wao wazo lao kubwa ni kupata ushindi tu hata uwe wa bao moja lakini Yanga wao wanataka ushindi tena mkubwa wa kuzidi zile 5-0 ili kuwaridhisha mashabiki wao na viongozi pia. Miwani yangu imechunguza na kutafakari kama hilo laweza kua ni mojawapo ya sababu iliyopelekea Yanga kupoteza mchezo huo.

· Usajili usio na Tija

Kuna vitu vingine viongozi wa timu hizi kubwa wanapaswa kubadilika hasa katika swala la usajili. Mara nyingi tumeona usajili umekua ukifanywa kuwafurahisha mashabiki bila kupata maoni ya kocha wa timu.
 

Yanga imemsajili Emmanuel Okwi hivi karibuni wakati huo huo

 

walishamrudisha kundini Mrisho Ngasa hii inaifanya Yanga kufikisha wachezaji wasiopungua 8 katika safu ya ushambuliaji hii inawapa faraja mashabiki lakini kwa timu haina tija. Jambo lingine linaloambatana na hilo ambalo mshikaji wangu Allen kaijage amelipinga ni kwamba wakati Usajili ukifanyika wanaosajiliwa wanalipwa pesa nyingi sana ikiwaacha waliopo sio tu wanalipwa kidogo lakini pia wanakosa namba hii kwa wachezaji Wabongo ambao hawajafikia "level" za Proffesionalism wanaweza kucheza chini ya kiwango ili kufikisha ujumbe kwa Uongozi.

Kwa haraka kabisa Miwani Pana ya Edo inaamini kua hizi ni kati ya sababu za chache kati ya nyingi ambazo pengine zimepelekea Yanga kupoteza mchezo wa Nani Mtani Jembe japokua makosa ya Uwanjani ndio yababu kubwa.

....... Imetayarishwa na Edo Daniel Chibo

Nitafute katika mfalme.edo@gmail.com au facebook Edo Daniel Chibo

 

No comments

Powered by Blogger.