KOMBE LA LIGI - MAN UNITED YATAKATA "YAJIANDAA KUKUTANA NA MAN CITY FAINALI"



Mabingwa watetezi wa Ligi kuu Nchini England klabu ya Manchester United Jana iliweza kujitengenezea mazingira mazuri ya kutwaa kombe la Ligi maarufu kama Capital One kwa kuibamiza Stoke City 2-0 mchezo uliopigwa katika dimba la Britania.

Mechi hiyo ambayo ilisimama kwa muda baada ya mvua kubwa kunyesha iliendelea baada ya mvua kukatika huku Man United wakipata goli la kwanza kupitia kwa Ashley Young kabla ya Patrice Evra kupigilia msumari wa ushindi kwa kufunga goli la pili akipokea pasi murua ya Ashley Young.

Katika mechi nyingine iliyopigwa katika jiji la London timu ya Totenham Hotspurs iliachwa midomo wazi baada ya kubamizwa 2-1 na West Ham kikiwa kipigo cha Pili mfululizo kwa Timu hiyo toka kwa West Ham katika uwanja wa White Hart Laine na kikiwa kipigo kingine toka ilipopata kipigo cha 5-0 toka kwa Liverpool kilichomfukuzisha kocha Andre Vila Boas

Spurs iliyobadilika toka katika benchi la Ufundi mpaka kikosi ilishuhudiwa ikicheza soka la kasi huku Emmanuel Adebayor na Jermain Defoe wakiongoza mashambulizi.
Adebayor aliipatia Spurs goli pekee baada ya kuunganisha mpira wa krosi ya Defoe kabla ya West Ham hawajazinduka na kurudisha goli hilo kupitia kwa Mathew Jarvis kabla ya Madibo Maiga hajamalizia kwa kufunga goli la ushindi.

Kwa matokeo ya Jana Man United na West Ham zimeungana na Man City na Sunderland kucheza hatua ya Nusu fainali ambapo Man United itakutana na Sunderland huku Mahasimu wao Man City wakikutana na West Ham United hali inayoonekana pengine tunaweza kuja kushuhudia Fainali kati ya mahasimu hao wa jiji la Manchester kama watafanikiwa kuvuka hatua ya nusu fainali.

Mechi za Nusu Fainali zitapigwa katika wiki inayoanzia Januari 6 na marudiano baada ya wiki mbili huku Fainali ikiwa mwezi Machi katika Dimba la Wembley.

No comments

Powered by Blogger.