KOMBE LA LIGI - CHELSEA YAANGUKIA PUA WAKATI MAN CITY IKIENDELEZA UBABE



 
Kikosi cha kocha Jose Mourinho jana kilijikuta kikiangukia pua katika mechi ya kombe la Ligi nchini England maarufu kama Capital one hatua ya Robo fainali baada ya kufungwa goli 2-1 dhidi ya Sunderland katika mchezo uliopigwa katika dimba la Sunderland (Stadium of Light)

Chelsea moja kati ya timu zilizopewa nafasi kubwa kuchukua ubingwa huo walipata bao lao la kwanza na la kufutia machozi dakika ya 46 goli la kujifunga la kiungo wa Sunderland Lee Cattermole alipotaka kuokoa mpira uliopigwa na Frank Lampard.
Mabadiliko yaliyofanywa na kocha wa Sunderland kuwaingiza Fabio Borini na kiungo mkorea Sung-Yueng Ki yalizaa matunda kwani Sunderland ilijipatia bao la kusawazisha kupitia kwa Fabio Borini dakika ya 89 na mchezo huo kumalizika kwa sare ya bao 1-1.

Muda wa Nyongeza ndio ulioimaliza Chelsea baada ya kiungo wa Sunderland Sung-Yueng Ki kufunga goli dakika ya 119, goli ambalo liliizamisha Chelsea na kuitoa kabisa katika michuano hiyo.

Man City kwa upande wao waliweza kuibuka na Ushindi wa 3-1 ugenini dhidi ya Leicester City magoli ya Alexandre Kolorov na magoli mawili ya mshambuliaji Edin Dzeko wakati goli la Leicester City likifungwa na Lloyd Dyer.

Mechi zingine za hatua hiyo ya robo fainali zitapigwa leo ambapo Man United watasafiri kuikabili Stoke City wakati Totenham watacheza na West Ham United.

No comments

Powered by Blogger.