LIGI KUU TANZANIA BARA ~ MBEYA CITY MAMBO YAZIDI KUWA MAZURI
Mzunguko wa 9 wa ligi kuu Tanzania Bara ulianza leo kwa viwanja vinne kuwa katika wakati mgumu ambapo timu iliyopanda daraja kutoka jiji la Mbeya timu ya Mbeya City imeweza kuchomoka na ushindi wa goli 1-0 dhidi ya Mgambo JKT katika mchezo uliopigwa katika jiji la Tanga hii inaifanya Mbeya City kupanda mpaka nafasi ya 3 katika msimamo wa ligi kuu Tanzania ikifungana pointi na Azam fc zote zikiwa na pointi 17.
Uwanja wa Azam Complex ulishuhudia mvua ya mabao kwa Azam kuwafunga JKT Ruvu mabao 3-0 magoli ya Humfrey Mieno,Erasto Nyoni na Sure Boy ushindi ambao ni mkubwa kwa Azam tangu kuanza kwa ligi hiyo na hii inawafanya Azam Kufikisha point 17 sawa na Mbeya City.
Mtibwa Sukari wao walikua nyumbani kuwaalika JKT Oljoro kutoka Arusha kwa kuwafunga magoli 5-2 katika mchezo mkali ulioshuhudia Abdallah Juma akiibuka mbabe wa kuzifumania nyavu baada ya kuondoka na mpira kwa kupika magoli matatu.
Ruvu Shootimg wakiwa mabatini mkoani Pwani waliwaalika Maafande wa Rhino Rangers ya Tabora na kuweza kuchomoka na ushindi wa bao 1-0 hivyo kuifanya Ruvu kufikisha pointi 13 katika nafasi ya 6.
KWA KIFUPI MSIMAMO WA LIGI KUU UKO HIVI
- Simba 18
- Azam fc 17
- Mbeya City 17
- Yanga 15
- Mtibwa Sukari 13
- Ruvu Shooting 13
- JKT Ruvu 12
- Coastal Union 12
- Kagera Sukari 11
- Prisons 7
- Rhino Rangares 7
- JKT Oljoro 6
- Ashanti 5
- Mgambo JKT 5
No comments