JE ETHIOPIA WATAFANIKIWA KUCHEZA KWA MARA YA KWANZA FAINALI ZA KOMBE LA DUNIA?
Mchakato wa Kutafuta wawakilishi watano wa bara la Afrika katika fainali za kombe la Dunia Nchini Brazil unaendelea katika hatua ya mwisho ambapo timu za mataifa 10 ya bara la Africa zinawania nafasi 5 za kuwakilisha bara hili.
Katika mechi zilizopigwa jana Jumamosi Bukinafaso wakiwa nyumbani waliweza kuwafunga Algeria 3-2 mechi kali ikipigwa katika jiji la Ouagadougou Nchini Bukinafaso magoli ya Bukinafaso yakiwekwa kimiani na Aristide Bance kwa penati, Djakaridja Kone na Jonathan Pitroipa huku magoli ya Algeria yakiwekwa kimiani na Sofiane Feghouli na Carl Medjani
Wababe wa Afrika katika soka Ivory Cost walifanikiwa kuifunga timu ngumu ya Senegal 3-1 nyumbani Didier Drogba akifunga mapema kwa Penati, badaye Ludovic Sane wa Senegal alijifunga kabla ya Solomon Kalou hajafunga goli la tatu huku goli la dakika ya Mwisho la Mshambuliaji wa Newcastle Papis Demba Cisse likiwa ni faraja kwa Senagal watakapokua wakijiandaa na mechi ya pili mwezi Novemba.
Leo Jumapili zitapigwa mechi mbili za hatua hiyo ambapo Ethiopia watakua nyumbani kujaribu bahati yao ya kucheza fainali za kombe la dunia kwa mara ya kwanza watakapowaalika mabingwa wa Afrika timu ya Taifa ya Nigeria katika mchezo utakaopigwa katika nchi yenye milima ya Ethiopia katika jiji la Adiss Ababa. swali ni kwanza Ethiopia wataweza kucheza kwa mara ya kwanza Fainali za kombe la dunia tena kwa kuwatoa mabingwa wa Afrika Nigeria?
Wakati huo huo Tunisia watakua nyumbani leo kuwakaribisha Cameron katika mchezo mwingine unaotarajiwa kuwa mkali
Mechi ya mwisho ya hatua hiyo itapigwa Jumanne ambapo Ghana wataialika Misri katika jiji la Kumasi huko Ghana.
Wachezaji wanaoongoza kwa kupachika mabao kwa upande wa Afrika mpaka sasa ni
Magoli 5
- Bernard Parker - Afrika Kusini
- Islam Sliman - Algeria
- Mohamed Salah - Misri
Magoli 4
- Yaya Toure - Ivory Coast
- Mohamed Aboutrika - Misri
....... Prepared by Edo Daniel Chibo
No comments