MIWANI PANA YA EDO ~ NI UAMUZI SAHIHI KWA OZIL KUJIUNGA ARSENAL KULIKO BALE KWENDA MADRID.
Wiki iliyopita ulimwengu wa Wapenda soka ulishuhudia rekodi mpya zikiwekwa katika usajili wa wachezaji mbali mbali duniani.
Kwa upande wa ligi kuu ya England rekodi mpya iliwekwa kwa mchezaji ghali zaidi duniani kununuliwa kutoka katika ligi hiyo pia rekodi nyingine mpya ya mchezaji ghali(kama sijakosea) kununuliwa akitoka nje ya ligi kuu England.
Pia ligi kuu England imeshuhudua zaidi ya Paundi milioni 600 sawa na euro milioni 700 zikitumika katika usajili wa wachezaji mbali mbali.
Kwanza kabisa ilikua ni Gareth Bale mchezaji bora wa ligi kuu England msimu uliopita akijiunga na Real Madrid kwa ada ya uhamisho wa Paundi Milion 85.3 ambayo ni kama Euro milion 100 akiweka rekodi mpya ya kua mchezaji aliyesajiliwa kwa pesa nyingi kuwahi kutokea duniani akimshinda Cristiano Ronaldo aliyekua akishikia rekodi hiyo tangu alipojinga na Madrid akitokea Man United pia ya England.
Pia tulishuhudia kwa mara ya kwanza baada ya minong'ono ya muda mrefu ya kumshinikiza kocha Arsene Wenger hatimaye Arsenal wakiweka rekodi yao katika klabu hiyo na rekodi katika ligi kuu England Msimu huu kwa kumsajili Mesut Ozil kwa ada ya uhamisho paund milion 42.5 sawa kama na euro milion 50 hivi.
Miwani yangu pana Jumapili ya leo ikiwa ni wikiend iliyopooza pengine kwakukosa msimimko wa mechi za ligi, najaribu kuangalia uamuzi upi ulikua sahihi hapa kwa wachezaji hawa wawili yani Bale aliyetoka EPL na Ozil aliyeingia EPL.
MESUT OZIL
Katika kikosi cha Real Madrid ulikua ukiwataja mastaa wa kikosi hicho basi ungeanza na Cristiano Ronaldo halafu wa pili ni huyu Jamaa. Mesut Ozil raia wa Ujerumani aliyejiunga na Madrid mwaka 2010 akitokea Werder Bremen ya Bundesliga.
Ni mchezaji mpole ambaye ukimchukia ni chuki zako tu binafsi. Huyu ni msingi mkubwa wa magoli ya Ronaldo tangu alipotua Madrid hili linathibitishwa na Ronaldo mwenyewe ambaye amesikitika jamaa kuondoka kwani ndo.mtu aliyekua akijua "movements" zake.
Baada ya kuona Gareth Bale amesajiliwa pale Madrid Ozil akaamua kufanya maamuzi sahihi yani kuihama klabu hiyo kwani ni ngumu mchango wake kuonekana kama angebaki hivyo akajiunga na Arsenal timu ambayo hakika Ikimuhitaji sio kwakua walikua na pesa za kumnunua lakini walimuhitaji ndani na nje ya uwanja(Makala ya The Gunning Machine imeshazungumzia jana).
Ozil amelamba dume kujiunga na Arsenal tofauti na kwamba angeenda Bayern Munich, Barcelona,Chelsea au PSG kwani uhakika wa namba katika kikosi cha kwanza ndani ya Arsenal ni 100%
Ozil anaingia katika kikosi cha Wenger ambacho amehangaika kukijenga kwa miaka karibia 10 iliyopita. Hapa naizungumzia Arsenal ambayo imeanza msimu mpya bila kumpoteza mchezaji yoyote wa kikosi cha kwanza hivyo Wenger alichokifanya ni kuongeza tu nguvu tofauti na miaka mingine ambapo alikua akitafuta mbadala wa mchezaji aliyeondoka.
Yani kwa maneno mengine Arsenal ya msimu huu Iko kamili.
Nionavyo mimi kwa kutumia hii miwani yangu pana huu ni mwaka wa Arsenal kufanya makubwa ndani na nje ya England na msaada mkubwa utakua kwa Ozil na pengine yaweza kua ni mwanzo wa Ozil kuja kuwa kama Thierry Henry (Nazungumzia heshima binafsi aliyopata Henry akiwa na Arsenal)
GARETH BALE
Kijana huyu mzaliwa wa Wales ambaye alijiunga na Totenham Hotspurs mwaka 2007 akitokea Southampton
Amejiunga na Real Madrid msimu huu akitokea Totenham Hotspurs kwa rekodi ya dunia ya uhamisho wa wachezaji. Paundi milioni 85.5 zimemng'oa kijana huyu Muingereza katika ligi kuu ya England kiwango ambacho kama mimi sidhani kama kinastahili kwa mchezaji ambaye hata Tuzo bora ya mchezaji wa Ukaya hajawahi kuipata.
Na hapa ndo huwa najiuliza, Kama Bale amenunuliwa kwa pesa hizo je vipi Messi angeuzwa kwa bei gani?
Anyway pengine Perez anajua zaidi lakini nikiangalia kwa makini nafasi ya Bale katika kikosi cha Real Madrid bado napata wasiwasi wa kile kitu ambacho Jamaa anapaswa kukifanya hapo ndo huwa narudisha lenzi za miwani yangu na kuangalia jinsi Michael Owen alivyopotea alipotua Madrid akitokea Liverpool ambako alikua staa.
Kiufundi wakati Bale yuko Spurs alikua ndo kila kitu yani penati alipiga yeye,kona yeye,free kicks yeye sasa anaingia katika kikosi cha Real Madrid ambacho wao wana Staa wao Cristiano Ronaldo huyu jamaa kama alivyokua Bale Spurs huyu ndo kila kitu Madrid na itaendelea kua hivyo kwani sioni namna Ronaldo anaweza kumwachia Bale akatawala wakati yeye yupo. Unadhani nini kitatokea uwanjani?
Bale anaenda katika timu iliyojaa mastaa na hasa katika safu ya ushambuliaji kwani ukimtoa Ronaldo wana Isco na Benzema pia ambao ao wana njaa ya magoli.
Ngoja tusubiri ila nionavyo mimi Gareth Bale atakua na presha kubwa sana ya kutaka kuuonyesha Ulimwengu na hasa mashabiki wa Real Madrid kama alistahili pesa hizo. Lakini utajiuliza pia kama Ronaldo anafunga magoli 50 kwa msimu je Bale atafunga mangapi ili awe juu ya Ronaldo na atayafungaje hayo magoli?
Namwangalia Bale ambaye wakati yuko Totenham alikua na majeruhi mara kwa mara na kila alipokua hayupo timu iliyumba hivyo kuvumiliwa na kuombewa arudi je Madrid ambao wako na presha kubwa ya kunyakua kombe la Mabingwa Ulaya ambalo hawajalipata tangu 2002 huku wakishindana kuwania La Liga dhidi ya Barcelona, wataweza kumvumilia?
Haya ni maswali ambayo hakuna anayejua majibu ni swala la muda tu kusubiri ila nadhani Bale itamlazimu kucheza hata akiwa majeruhi ili kukonga nyoyo za mashabiki ambao wana kiu ya kuangalia nini atafanya zaidi ya kile wanachokipata kwa Cristiano Ronaldo.
Japokua kuna mawzo mengi yanakuja katika vichwa vya wapenda soka kama Gareth Bale bado ni mdogo yani kwa umri alionao wa miaka 23 anaweza kupigania namba ila swali linabaki Madrid wako tayari kumvumilia wakati sera ya Rais wa Madrid Perez ni kununua mastaa. Naona wakati Bale akipigania Namba akatokea mkali mwingine ambaye atanunuliwa pia na kuingia moja kwa moja katika kikosi cha Madrid.
Kuna timu ambazo zinanunua wachezaji kwa mategemeo ya kukaa nao kwa muda mrefu lakini silioni jambo hilo katika Real Madrid.
Mshkaji wangu David Samuel Marosi wa wapenda Soka group yeye anaamini kama kitu pekee ambacho Madrid wangefanikiwa ni kumpa timu kocha Arsene Wenger halafu saizi wangekua tishio Ulaya na Spain na hili linatokana na uwezo wa kocha huyo katika kutengeneza timu imara katika bajeti ndogo. Yani yuko kama Mimi kama kikosi cha Kocha Jose Mourinho kilichokua na kila kitu kikachemka itakuaje hiki cha Ancellot?
Kwa kutumia miwani yangu hii pana yenye lensi nyekundu nathubutu kusema haukua uamuzi sahihi kwa Bale kujiunga na Madrid ndani ya uwanja ila kwa nje ya uwanja poa sana kwake kwani hata mimi ningesaini kuichezea Madrid kwa mshahara wa paundi laki 3 kwa wiki si mchezo.
Kwa leo naishia hapa ila unaweza kunicheki kwa maoni na ushauri kwa
email: wapendasoka@gmail.com
Faceboo: Edo Daniel Chibo
Facebook page: Wapenda Soka - Kandanda
Mobile: 0762 42 7272
No comments