FULHAM VS ARSENAL ~ JE REKODI MBAYA KWA ARSENAL TANGU KUANZISHWA LIGI KUTIMIA LEO?
Arsenal wanaingia katika dabi ya mji wa London leo na safari hii watapambana na Fulham katika uwanja wa Craven Cotage katika mechi itakayoanza saa 9 kasorobo saa za hapa Bongo. Huku ikiwa na rekodi ya kutopoteza mechi mbili mfululizo za mwanzo wa ligi tangu EPL ilipoanzishwa.
Hii ni mechi ya pili tangu kuanza kwa ligi kwa timu zote mbili huku Arsenal wakiingia uwanjani wakiwa na kumbukumbu mbaya ya kufungwa 3-1 katika mechi ya Ufunguzi dhidi ya Aston Villa huku Fulham walianza ligi vizuri wakipata ushindi wa 1-0 ugenini dhidi ya Sunderland.
Huku mashabiki wengi wa Arsenal wakipoteza matumaini katika swala zima la Usajili kwani mpaka sasa ni Yaya Sanogo tu aliyeongezwa kikosini, Fulham wao wameongeza baadhi ya wachezaji akiwemo Scott Parker toka Totenham Hotspurs na Darren Bent aliyejiunga na Fulham kwa mkopo akitokea Ason Villa.
Safu ya ushambuliaji ya Arsenal Inamtumia Olivier Giroud ambaye anaonekana kuimarika kadri siku zinavyozidi kwenda kwani katika mechi 49 alizoichezea Arsenal mpaka sasa kafunga magoli 19 alifunga magoli mawili katika mechi dhidi ya Fulham msimu uliopita pale Emirates. Atasaidiwa na Theo Walcott japokua tatizo litakua katika nafasi ya ulinzi ambapo Arsenal inaingia katika mchezo wa leo ikiwa na beki mmoja tu Per Metasacker wa nafasi ya kati na kuna tetesi pengine Bakary Sagna akacheza nafasi hiyo ya kati.
Golikipa wa Fulham Maarten Stekelenburg aliumia bega katika mechi dhidi ya Sunderland hivyo David Stockdale ataanza katika mechi hiyo wakati kwa upande wa mbele utaongozwa na Dimitar Berbatov na Bryan Ruiz
Kwa upande wa Arsenal Laurent Koscielny ataikosa mechi hiyo kutokana na kadi nyekundu aliyoipata walipocheza na Aston Villa wakati Nacho Monreal amerudi kikosini huku Alex Oxlade-Chamberlain akiungana na Thomas Vermaelen katika orodha ya majeruhi.
KUMBUKUMBU MUHIMU
- Arsenal haijawahi kupoteza mechi mbili mfululizo za ufunguzi wa ligi tangu ligi kuu kuanzishwa miaka 21 iliyopita huku Fulham haijawahi kushinda mechi mbili mfululizo za msimu mpya wa ligi tangu msimu wa 2000/2001 walipopanda daraja na kushinda mechi 11 mfululizo.
- Mechi 3 kati ya 5 zilizopita baina ya timu hizo ziliisha kwa matokeo ya Sare.
- Fulham wameshinda mechi tatu tu kati ya 24 ambazo zimezikutanisha timu hizo katika ligi na mechi zote hizo 3 walizoshinda ilikua katika uwanja wa Craven Cotage.
- Tangu Fulham waliporudi katika ligi kuu Arsenal imeshinda mechi 8 kati ya 12 katika uwanja wa Nyumbani wa Fulham.
- Mechi tatu za mwisho kati ya timu hizo katika uwanja wa Craven Cotage zilizalisha kadi nyekundu 4.
- Katika mechi 8 alizocheza Darren Bent dhidi ya Arsenal amefunga magoli 6
- katika dabi zote za London msimu uliopita Arsenal waliweza kupata pointi 19 nyingi zaidi ya timu yoyote katika jiji la London.
- Ukiacha Manchester City iliyofungwa magoli 34 msimu uliopita ni Arsenal pekee ndo ilifungwa magoli machache zaidi ya timu zingine ikifungwa magoli 37.
- Olivier Giroud amefunga magoli 12 mpaka sasa katika ligi na magoli yote hayo ameyafunga akiwa London 11 yakiwa katika uwanja wa Emirates.
- Arsenal wamepata kadi nyekundu nyingi zaidi ya timu yoyote katika Ligi kuu tangu kuanza kwa msimu uliopita mpaka sasa Arsenal wamepata kadi nyekundu 6.
MECHI ZINGINE KATIKA EPL LEO
- Everton v West Bromwich Albion 5pm
- Hull City v Norwich City 5pm
- Newcastle v West Ham United 5pm
- Southampton v Sunderland 5pm
- Stoke City v Crystal Palace 5pm
- Aston Villa v Liverpool 7:30pm
No comments