MECHI MAALUMU KWA RIO FERDINAND ~ USAIN BOLT NA RONALDO UWANJANI?
Leo katika uwanja wa Old Trafford nyumbani kwa Mabingwa wa England Manchester United kutakua na mechi ya heshima kwa beki wa timu hiyo Rio Ferdinand akitimiza miaka 10 ndani ya mabingwa hao na huu ukiwa ni mwaka wake wa 11 kuitumikia timu hiyo.
Rio mwenye umri wa miaka 34 alijiunga na Man United mwaka 2002 akitokea Leeds United kwa ada ya uhamisho paundi milion 30 na kumfanya kuwa mchezaji aliyenunuliwa kwa pesa nyingi zaidi ambaye ni raia wa England na kumfanya kuwa beki ghali kabisa duniani.
Rio ambaye ni baba wa watoto watatu atakiongoza kikosi cha Man United kucheza na Sevilla ya Hispania katika mechi itakayoanza saa 3:30 usiku huku kukiwa na tetesi nyingi kuhusu wachezaji watakaoichezea Man United hii leo.

Mengi tutayashuhudia muda huo lakini hii si mechi ya kukosa kuitazama.
Rio Ferdinand anaingia katika msimu wake wa 11 hivi sasa huku akiisaidia klabu hiyo kushinda mataji 6 ya Ligi kuu England akicheza mechi 297 na kufunga magoli 7
Ameshinda kombe la Ligi mara 2, Ngao ya Hisani mara nne, Klabu bingwa Ulaya mara moja na Kombe la klabu bingwa ya dunia mara moja.

Sir Alex Ferguson aliiambia website ya klabu hiyo kama Rio ni kati ya mabeki bora kuwahi kutokea katika historia ya klabu hiyo
Manchester United itacheza na Wigan Jumapili katika ngao ya jamii na ufunguzi rasmi wa msimu mpya wa Ligi kuu England katika uwanja wa Wembley.
>>>>> Imeandikwa na Edo Daniel Chibo wa Wapenda Soka (kandanda) group katika Facebook
No comments