MECHI YA KWANZA OLD TRAFFORD MOYES AANZA NA KICHAPO
Rio akiwa na wanawe watatu |
Kama ilivyokua kwa mechi yake ya kwanza akiwa kama Kocha wa Man United alipofungwa na kombaini ya Sigha vivyo hivyo mechi ya kwanza ya kocha huyo katika uwanja wa Nyumbani wa Man United, Old Trafford amefungwa 3-1 na timu inayoshiriki ligi ya Spain Sevilla.
Gwaride la heshima kwa Rio |
Japokua ilikua ni mechi ya kirafiki ya shukrani kwa beki wa timu hiyo Rio Ferdinand lakini United iliingiza kikosi cha wachezaji wake wote ambao iko nao msimu huu huku Kocha David Moyes akiwa benchi na kuifanya mechi hiyo kuwa ni muhimu katika maandalizi ya msimu mpya tofauti na wengi tulivyofikiri kama kungekua na mishangao "suprises" kwa kushuhudia watu kama Usain Bolt ambaye alipambwa na magazeti ya England kuwa angecheza mechi hiyo.
Hatujui nini kilitokea nyuma ya pazia lakini mechi ilikua na msisimko wa aina yake hasa kwa vinaja United.
Mpaka Mapumziko United walikua washalala 2-0 magoli ya Vitolo na mchezaji wa Chelsea Marko Marin kabla ya Valencia hajaifungia United goli la kufutia machozi dakika ya 65.
Rabello alipigilia msumari wa machungu dakika ya 92 alipofunga goli la Tatu.
Katika mchezo huo United waliwapumzisha wachezaji kadhaa wa kikosi cha kwanza hasa upande wa Ushambuliaji na kinda wa Chile Angelo Henriquez alianza kama mshambuliaji wa mwisho akisaidiana na Shinji Kagawa huku dimba la kati likimilikiwa na Anderson .
Nyuma alikuwepo De Gea mabeki wake wakiwa ni Fabio kulia na Buttner kushoto wakati kati alikuwepo Rio Ferdinand na Chriss Smalling.
Katika mechi hiyo kiungo mshabuliaji raia wa Ubelgiji Adinan Januzaj alizawadia heshima ya kua mchezaji bora wa mechi hiyo
Kesho Jumapili United wataingia katika uwanja wa Wembley kama Mabingwa watetezi EPL wakiumana na mabingwa wa kombe la FA klabu ya Wigan ambao wanacheza katika Championship mwaka huu.
Mchezo huo utakua ni wa ngao ya jamii na ufunguzi rasmi wa ligi kuu msimu mpya kat ya mabingwa wa Ligi na mabingwa wa kombe la FA.
No comments