CHELSEA HOI KWA MADRID, RONALDO APIGA MBILI



Mabingwa wa kombe la Europa klabu ya Chelsea imejikuta ikiangukia pua baada ya kupigwa 3-1 katika mashindano ya Guiness International Champions Cup yaliyomalizika Alfajiri  nchini Marekani

Katika mechi hiyo iliyopigwa kuanzia saa 10 Alfajiri kwa saa za Afrika Mashariki ilishuhudia kocha aliyeihama Real Madrid Jose Mourinho akiikabili timu aliyokua nayo msimu uliopita huku Carlo Ancelott kocha wa Real Madrid akikutana na timu yake ya zamani Chelsea.

Ilikua mechi kali ya kusisimua huku Real Madrid wakipata goli la kwanza dakika ya 14 kupitia kwa beki raia wa Brazil Marcelo kabla ya Ramires hajaisawazishia Chelsea dakika 2 baadaye yani dakika ya 16.
Dakika ya 31 Cristiano Ronaldo alipiga goli safi na kuifanya Madrid kwenda mapumziko wakiwa mbele kwa goli 2-1. Dakika ya 57 krosi safi iliyopigwa na winga mshambuliaji Isco iliunganishwa vizuri na Cristiano Ronaldo na kuandika bao la 3 lililoizamisha Chelsea ambayo ilionekana kupotea kipindi cha pili.

Ronaldo amemfunga mdomo kocha Mourinho ambaye wiki iliyopita alimzungumzia vibaya Ronaldo aliposema kama Ronaldo wa kweli ni yule Mbrazil pekee hali iliyochukuliwa kama dharau kwa Cristiano Ronaldo.

Fernando Torres na Victor Mosses walishindwa kabisa kumalizia nafasi za wazi walizozipata huku kipa Ike Casillas akionekana shujaa baada ya kucheza hatari kadhaa ambazo zingezaa magoli.
Mechi hiyo imekua ya kwanza kwa kocha Jose Mourinho kupoteza katika mechi za maandalizi ya msimu mpya wa ligi.

Kwa matokeo haya Real Madrid wamekua mabingwa wa michuano hiyo nafasi ya Pili huku AC Milan ikishika nafasi ya Tatu baada ya kuifunga LA Galaxy 2-0 katika mechi iliyopigwa mida ya saa 7 usiku. Nafasi ya nne inakamatwa na LA Galaxy huku nafasi ya Tano ikikamatwa na Valencia,Everton nafasi ya Sita, Inter Milan ya 7 huku Juventus wakikamata mkia.

~~Edo

No comments

Powered by Blogger.