THE GUNNING MACHINE ~ WATAZAME HAWA KWA JICHO LA TATU. KUNA SIKU UTAKUMBUKA MANENO YANGU.
Wapenzi wa The Gunning Machine ya Wapenda Soka, leo sitaki kuzungumza kitu kuhusu usajili. Na hata wiki ijayo sitazungumza usajili pia.
Unamkumbuka Jacky Wilshere wa zamani? Alijiunga na shule ya soka ya Arsenal akiwa mtoto kabisa lakini leo ni mchezaji mkubwa. Nataka tuwatazame vijana ambao wanaonesha dalili njema za kuja kuwa wachezaji hatari kwa siku za usoni.
IGNASI MIQUEL
Kijana wa Kihispaniola aliyezaliwa Septemba 28, 1992.
Ni beki wa kati mwenye uwezo wa kucheza pia kama beki wa kushoto.
Miquel ni zao la shule ya soka ya Barcelona La-masia. Alidumu kwa miaka mitano huko kabla ya kuhamia katika klabu ya UE Cornella ambako kiwango chake kilimfanya kuonekana na kupewa nafasi ya kufanya majaribio na Arsenal.
Alijiunga na Arsenal katika msimu wa 2009/2010 na kupewa unahodha wa kikosi cha wachezaji wa akiba akicheza jumla ya michezo 12.
Msimu wa 2010/2011, Miquel alicheza michezo kadhaa ya kombe la ligi pamoja na kombe la FA.
Aliendelea kufanya vizuri katika msimu wa 2011/2012 ambapo alihusishwa katika michezo michache ya ligi kuu na ile ya ligi ya mabingwa Ulaya.
Kiwango chake kinakua na anaweza kupata nafasi zaidi msimu ujao. Ni mchezaji wa kumtazama, amechezea ngazi zote za timu za taifa za vijana za Hispania.
SERGE GNABRY
Mjerumani mwenye mama wa Ki-ivory coast. Alizaliwa Julai 14, 1995 katika mji wa Stuttgart huko Baden-Wurtenberg nchini Ujerumani. Alianza maisha yake kama mwanariadha, lakini alitakiwa kuchagua kati ya riadha na soka na soka ikawa chaguo lake.
Arsenal walimpata kutoka VfB Stuttgart kwa kiasi cha £100,000 tu ambazo ni sawa na mshahara wa Theo Walcott kwa wiki.
Alijiunga na Arsenal mnamo mwaka 2011 na kujiunga na kikosi cha vijana chini ya miaka 18 kabla kuingia katika kikosi cha wachezaji wa akiba wa Arsenal ambako alifanikiwa kufunga mabao mawili katika michezo 6.
Msimu wa mwaka 2012/2013 ulikua mzuri kwa Gnabry kwani aliingia kwenye kikosi cha kwanza cha Arsenal na kucheza michezo michache ukiwemo ule wa ligi kuu dhidi ya Norwich City ambapo Arsenal walikubali kichapo cha bao 1-0 ugenini.
Mchezo huo ulimfanya Gnabry kushika nafasi ya tatu kama mchezaji mdogo wa Arsenal kucheza ligi kuu nyuma ya Cesc Fabregas na Jack Wilshere.
Siku nne baadae, Gnabry aliichezea Arsenal mchezo wa ligi ya mabingwa dhidi ya Schalke 04 ya Ujerumani, Arsenal ikikubali kichapo cha bao 2-0 nyumbani.
Ana kasi na nguvu. Ni kijana wa kumtazama sana kwa siku za usoni. Anaichezea timu ya taifa ya Vijana chini ya miaka 18 ya Ujerumani.
CHUBA AKPOM
Mshambuliaji kijana lakini mpambanaji mwenye nguvu. Ana uwezo wa kucheza nafasi zote za ushambuliaji. Ni hazina ya nguvu ya Arsenal.
Akpom alizaliwa Oktoba 9, 1995.
Aliichezea timu ya vijana ya Arsenal chini ya miaka 18 na kufanikiwa kufunga mabao 2 katika michezo 15.
Chuba ni mali ya timu ya taifa ya vijana ya England na anatazamwa kama kinara wa baadae.
THOMAS EISFELD
Anatajwa kama mrithi sahihi wa Cesc Fabregas. Alizaliwa Januari 8, 1993. Alianza soka lake katika klabu ya Borussia Dortmund japo aliwahi kucheza katika vilabu vingine vidogo vidogo hapo kabla.
Alijiunga na Arsenal Januari 31, 2012 kwa ada ya £475,000.
Alipata nafasi ya kukicheza kikosi cha kwanza cha Arsenal katika ule mchezo wa kombe la ligi dhidi ya Reading, Arsenal wakishinda kwa mabao 7-5 katika muda wa nyongeza.
Ameonesha kiwango kizuri katika michezo ya majaribio msimu huu na una sababu ya
kumtazama kwa jicho la tatu.
GIDION ZELALEM
Nitaamini hata Ulaya kuna misumari kama kijana huyu hatokuwa staa miaka kadhaa ijayo. Ni kijana hatari sana, ana umri wa miaka 16 tu lakini kiwango chake kinashitua wengi.
Zelalem anacheza kama kiungo mshambuliaji, anajua kushambulia lakini pia ni fundi mzuri wa pasi za mwisho.
Wengi wameukubali uwezo wake katika mechi cha majaribio msimu huu. Bila shaka kuna mengi mazuri kutoka kwa kijana huyu wa kijerumani mwenye asili ya Ethiopia.
BENIK AFOBE.
Mshambuliaji wa Kiingereza aliyezaliwa Februari 10,1993. Alijiunga na academy ya Arsenal akiwa na miaka 6 tu.
Alishitua kwa kufunga magoli 40 akikichezea kikosi cha U16 cha Arsenal msimu wa 2007/2008.
Kisha akafunga mabao 11 katika michezo 13 msimu wa 2008/2009.
Afobe aliifungia Arsenal U18 mabao 21 katika michezo 24 msimu wa 2009/2010 kabla ya kusaini mkataba wa kulipwa na Arsenal baada ya tetesi kuwa anatakiwa na Barcelona.
Alicheza kwa mkopo Huddersfield Town msimu wa 2010/2011.
Machi 2012 akajiuna na Reading kwa mkopo mpaka mwisho wa msimu.
Agosti 2012 akajiunga na Bolton Wonderes kwa mkopo wamuda mrefu lakini mkataba ulisitishwa na akajiunga na Millwal lakini akapata majeraha ya goti yaliyomsabisha kurejea Arsenal.
Amezichezea ngazi zote za timu za vijana za England. Nadhani amepata uzoefu wa kutosha na ni muda wa kumtazama kwa makini.
Tukutane tena wiki ijayo.
>>>>>>>>>>>>>>>>>>>......
Imeandikwa na Richard Leonce Chardboy kutoka Wapenda Soka(Kandanda) Group katika Facebook.
Nipate katika chardboy74@gmail.com na @chardboy77 kwenye twitter. Au 0766399341

No comments