LIGI YA MABINGWA ULAYA ~ CELTIC NA LYON WAAMBULIA VICHAPO HUKU AC MILAN WAKIVUTWA SHATI
Hatua ya mtoano ya ligi ya mabingwa Ulaya msimu huu imeanza huku ikishuhudia bingwa wa Historia wa Ligi hiyo AC Milan wakivutwa shati na kulazimishwa sare ya 1-1 na PSV ya Uholanzi ikiwa ni mechi ya kwanza kati ya mbili za kucheza katika nafasi ya makundi kukamilisha timu 32.
Katika mechi hiyo iliyomrudisha mshambuliaji wa zamani wa timu ya PSV na Man United Ji Sung Park, Milan walianza kupata bao kupitia kwa Stephan El Sharaawy kabla ya Tim matavz kusawazisha akimalizia mpira uliotemwa na kipa wa Milan baada ya Bruma wa PSV kupiga shuti kali.
Katika Mechi nyingine Celtic ikisafiri ugenini ilikubali kichapo cha 2-0 toka kwa Shakhter Karagandy na kuifanya mechi ya marudiano wiki ijyo kua ngumu kwa mabingwa hao wa ligi kuu Scotland.
Magoli ya Shakhter yalifungwa na Finonchenko na Khizinhincheko huku Cetic wakikosa magoli ya wazi katika mchezo huo.
Olimpic Lyon wao walikubali kichapo cha 2-0 toka kwa timu ya Real Sociedad ya Spain katika mchezo uliochezwa katika jiji la Lyon nchini France
magoli ya Antoine Griez na Haris Seferovic
Katika mechi zingine Victoria Plzen wakiwa nyumbani waliwapa kichapo Maribor cha mabao 3-1 huku P. Vereira ikilambishwa 4-1 na Zenit
Ligi hiyo itaendelea kesho huku kukiwa na mechi nyingine nyingi zitakazopigwa katika viwanja mbali mbali japokua macho na masikio yatakua huko Instabul kuishuhudia Arsenal ikicheza dhidi ya Fernabahce.
No comments