CHELSEA vs ASTON VILLA ~ HISTORIA INAWAPA USHINDI CHELSEA


Chelsea inaikaribisha Aston Villa usiku huu katika mechi ambayo ni vigumu kutabiri japo wengi wanaipa nafasi Chelsea kushinda
Villa ambao wanaingia katika mchezo wa leo wakiwa na kumbukumbu nzuri ya kuanza ligi vizuri baada ya kuifumua Arsenal 3-1 hapo hapo London.
Mara ya mwisho kwa Aston Villa kucheza katika dimba la Stamford Bridge walifungwa goli 8-0.
Juan mata, Andre Schurrle,Demba Ba na Lukaku wanatarajia kuanza katika mechi ya leo kwa upande wa Chelsea.

HISTORIA

Mara ya mwisho Villa kuingia katika uwanja wa Stamford Bridge walikubali kupokea kipigo kinachoaminika ni cha kwanza tangu kuanzishwa kwa klabu hiyo kwani walifungwa 8-0.

Katika mechi nne walizokutana katika Ligi Chelsea kashinda mechi tatu na kupoteza moja na kufunga magoli 14
Katika mechi 11 za Villa kucheza Stamford Bridge wameweza kushinda mechi moja tu wakipoteza mechi 7.

Jose Mourinho hajawahi kupoteza mchezo wowote wa ligi katika uwanja huo kwani katika mechi 61 Imeshinda 47 na kutoa sare 14.

Katika mechi nne dhidi ya Mourinho na Chelsea Yake Ametoka sare 3 na kupoteza mchezo mmoja.

Aston Villa hawajafungwa katika mechi tatu za ugenini katika ligi kuu England Tangu walipofungwa mara ya mwisho 3-0 na Manchester United.

Villa ndo timu pekee ambayo imepata pointi nyingi za Ugenini (point 21) kuliko nyumbani (point 20) katika msimu ulioisha

KOCHA JOSE MOURINHO

kocha Jose Mourinho amecheza michezo 61 ya ligi katika uwanja wa nyumbani wa Chelsea akishinda 47, Amedroo 14 na hajapoteza mchezo wowote. Huku akifunga magoli 125 akifungwa magoli 28 tu huku akijikusanyia pointi 155 kati ya 183 alizopaswa kuzipata katika michezo hiyo.

Mechi inaanza saa 3:45 Usiku huu.

No comments

Powered by Blogger.