HUU NI UTANI! PAUNDI MILION 105 KWA GARETH BALE?

Kocha wa Arsenal mfaransa Arsene Wenger anaamini kutoa paundi milioni 105 kumsajili Gareth Bale ni utani katika soka.
Wenger amezinyoshea kidole klabu zote ambazo zinazotumia pesa nyingi katika kusajili kama zitaathirika sana na sheria itakayoanza kutumia msimu huu ya kila klabu kusajili kutokana na pesa wanazozalisha na kubalansi vitabu vyao.

Arsene Wenger akiwa na kocha msaidizi Steve Bould
Anaamini Gareth Bale ni mchezaji mzuri lakini si kwa kiasi hicho cha pesa na japokua Spurs ni wapinzani wao wakubwa katika soka lakini amesema angependa Bale abaki na kuendelea kucheza katika ligi kuu England.
" Si vizuri kupoteza wachezaji bora, Ni Muingereza ingekua muhimu Ligi kuu England ingewatunza nyota wa ligi hiyo" Alisema Wenger

Real Madrid wameweka mezani kiasi cha paundi milion 105 pamoja na mshahara wa Paundi 165,000 kwa wiki zikiwemo allowansi na bonasi ili kumnyakua staa huyo raia wa Wales ambaye alikua nyota wa klabu ya Totenham Hotspurs na ligi kuu England msimu ulioisha.

Kama Real Madrid watafanikiwa kumsajili Bale kwa kiasi hicho cha pesa watakua wamevunja rekodi ya Usajili waliyoiweka walipomsaji Cristiano Ronaldo kwa paundi milion 80 kutoka Manchester United hivyo kumfanya kuwa mchezaji ghali zaidi ya Ronaldo ambaye anashika rekodi hiyo.

Wenger anashangazwa kuona pesa nyingi zinatumika katika kusajili katika mwaka ambao sheria ya matumizi bora ya Rasilimali za klabu itakapoanza kutumika na kila klabu kutumia pesa zinazotokana na faida ya klabu.
Inasemekana Arsenal wamempa Arsene Wenger paundi milion 120 ili kusajili msimu huu lakini mpaka sasa Wenger amemsajili mshambuliaji kinda raia wa Ufaransa Yaya Sanogo kwa uhamisho huru kutoka klabu ya Auxerre ya Ufaransa.

Huku kukiwa na minong'ono mingi kuhusu Arsenal kutaka kumsajili mfungaji bora wa Liverpool msimu ulioisha Luis Suarez huku Wenger akimtahadharisha Suarez na wote wanaotaka kuhamia Arsenal kama lazima waheshimu Utamaduni wa klabu ambao umejengwa kwa zaidi ya miaka 130 sasa.

Mwaka huu imeshuhudiwa pesa nyingi zikitumika katika usajili kwa klabu tofauti tofauti kwani PSG wamemsajili Edsoni Cavani kwa Paundi Milion 55 wakati Barcelona wakimsajili Neymar kwa zaidi ya paundi milioni 50
huku Manchester City wakitumia zaidi ya Paundi milioni 90 katika usajili wao.
Huku Monaco wakitumia zaidi ya paundi milioni 120 katika usajili.

Tunaendelea kusubiri kuona nini kitatokea kwa Bale lakini kuna kila sababu za kuamini kama Gareth Bale atavaa "uzi" wa Real Madrid msimu huu mpya.

1 comment:

Powered by Blogger.