SIMBA,LIVERPOOL,ARSENAL,GALATASARAY, MAN UNITED NA PSG WOTE UWANJANI LEO

Ikiwa leo ni Tarehe 3 Agosti, maandalizi ya msimu mpya wa ligi yako katika hatua za mwisho kwa timu mbalimbali duniani kujaribu vikosi vyao ikiwa ni pamoja na kuangalia wachezaji wapya waliosajiliwa watacheaji na waliopo ili kuleta chachu ya Ushindi.
Mechi nyingi zinapigwa leo duniani ikiwa ni mwendelezo wa kujiandaa na ligi mbalimbali na hapa tumezikusanya zile mechi zenye kugusa mashabiki wengi.


SIMBA SPORTS CLUB


Baada ya kupoteza ubingwa wao dhidi ya watani zao Yanga msimu uliopita, Klabu ya Simba imefanya mabadiliko makubwa katika kikosi chake na benchi la Ufundi kwa kumrudisha nguli wa klabu hiyo Abdallah Kibaden kama kocha mkuu akisaidiwa na Jamuhuri Kiwelu "Julio" leo wataingia uwanja wa Taifa kumenyana na Timu ya Taifa ya Tanzania kwa upande wa majeshi kuanzia saa 10 jioni.
Kikosi kilichosheheni vijana weng ndo kinachotarajiwa kucheza katika msimu huu kwa upande wa Simba pia itakua na beki wake aliyerudi kundini Joseph Owino ambaye aliwahi kutemwa siku za nyuma.
 
                                ARSENAL FC

Jiji la London leo litashuhudia miamba minne kutoka ligi nne barani Ulaya wakimenyana kuwania kombe la Emirates ambalo huandaliwa na klabu ya Arsenal na wadhamini wakuu wa klabu hiyo kampuni ya ndege ya Fly Emirates

Miamba itakayojitupa leo katika uwanja wa Emirates ni wenyeji Arsenal, mabingwa wa Uturuki Galatasaray,Mabingwa Wa Ureno FC Porto na klabu ya Napoli ya Italia inayofundishwa na kocha Rafael Benitez.

Mchezo wa kwanza utakua kati ya Galatasaray dhidi ya FC Porto mida ya saa 10 jioni ukifatiwa na ule wa Arsenal dhidi ya Napoli mida ya saa 12:20 jioni.

                 

                         LIVERPOOL FC

Magwiji wa Liverpool Jermie Carragher na Robie Fowler watarudi uwanjani Enfield leo katika mechi ya shukrani kwa Nahodha Steven Gerrard mechi itakayoanza saa 8:45 mchana dhidi ya Olympiakos ya Ugiriki
Mechi hii ni maalumu kwa Gerard kutokana na unahodha uliotukuka katika Liverpool na msaada wake mkubwa katika klabu hiyo tangu alipoanza kuichezea miaka 15 iliyopita.

Gerard ni kati ya wachezaji wachache waliofanikiwa kuicheza timu moja katika maisha yao ya soka.



      MANCHESTER UNITED

Unaweza ukaitafuta katika ratiba usiikute habari ya Man United kucheza leo lakini ni kweli kikosi cha wachezaji wa akiba wa Mabingwa wa England kikijumlisha na wale wa kikosi cha kwanza waliokua majeruhi Kitashuka leo kumenyana na Real Betis.
United leo kutoka katika kikosi cha kwanza watakuwepo Wayne Rooney,Nemanja Vidic,Antonio Valencia,Luis Nani na Javier Hernandez "Chicharito" hii ni kuwaweka vizuri wachezaji hao kabla hawajaungana na Wenzao wa kikosi cha kwanza siku ya Jumanne watakapocheza mechi ya kirafiki dhidi ya AIK ya Sweden huko katika jiji la Stockholm kabla ya Ijumaa kucheza mechi maalumu ya Shukrani kwa Rio Ferdinand katika uwanja wa Old Trafford.



             PARIS SANT GERMAIN (PSG)

Ufunguzi wa Ligi kuu Ufaransa utakua leo mida ya saa 3:45 usiku katika jiji la Libreville nchini Gabon kati ya mabingwa wa Ligi kuu Ufaransa klabu ya PSG wakiumana na bingwa wa kombe la ligi Ufaransa klabu ya Bodeaux.
 Baada ya kutumia paundi milion 55 kumsajili mshambuliaji raia wa Uruguay PSG inapewa nafasi kubwa kushinda mechi hiyo.

1 comment:

Powered by Blogger.