VIPANDE THELATHINI VYA YUDA ISKARIOTE NDANI YA MFUKO WA KASEJA


Juma Kaseja
Usaliti ni kitu kibaya sana.Hakuna mtu anayependa kusalitiwa pia hakuna mtu anayependa kusaliti. Kila kitu hutokea kwasababu na ndio maana usaliti hutokea kwa sababu.Usaliti haukuanza jana,usaliti ulikuepo,upo na utaendelea kuepo.

Wengi wetu tunamfahamu Yuda Iskariote.Mfuasi wa Yesu ambaye baadaye alimsaliti.Yuda iskariote hakumsaliti yesu bure,Yuda iskariote hakutosheka na maisha aliyokuwa akiishi,Yuda iskariote alihitaji fedha kama mimi na wewe tunavyohitaji.Vipande thelathini vya fedha alivyopewa Yuda vilitosha kumsaliti YESU.Oooops kumbe Yuda alimsaliti YESU kwasababu ya fedha?.
Fedha kweli mwana haramu,Fedha ndio chanzo kikuu cha usaliti.Watu wengi wameua ndugu zao kwasababu ya fedha,Wengi wamewasaliti wapenzi wao kwasababu ya fedha.

Huku kwetu kwenye soka kidudu usaliti kimetapakaa kwa kasi.Sababu ni ileile fedha.Ulaya,bongo na Dunia kwa ujumla.Wengi tunamfahamu Anelka,unajua kwanini aliondoka Arsenal?Jibu ni moja tu fedha.Arsenal walimuhitaji sana Anelka,lakini yeye mwenyewe akalazimisha kuondoka akatafute maisha bora,akaenda zake Madrid ambako hata hivyo hakudumu.

Kuna mfaransa mwingine anaitwa samir nasri,nae kama ndugu yake anelka aliomba kuondoka arsenal huku akieleza sababu tele ila ya moyoni ilikua fedha.Wachezaji hao wote ni matunda ya arsene wenger,wenger ndiye alifanya Samir Nasri na Anelka wajulikane kama wachezaji,lakini mwisho wa siku vijana hao wakamkacha babu wenger na kwenda kuogelea pesa

Pia kwetu bongo kisa ni kile kile na sababu ni ile ile.Mwaka 2008 kipa namba moja wa simba na taifa stars juma kaseja,aliikacha simba na kusaini jangwani.Sababu ya kaseja ilikua ni ile ile maslahi.Sina uhakika kama Simba walishindwa kumtimizia matakwa yake au yeye alihitaji zaidi ya hilo?.Nani ajui kua simba ndo ilomfanya kaseja aitwe kaseja? Mwaka 2008 kaseja alivyoenda yanga wote tulimsapoti kwa kusema yeye kama mchezaji lazima aangalie maslahi yake kwanza.Lakini leo kila mtu anawanyooshea viongozi wa simba vidole.

Hivi nani ajui kama kiwango cha Kaseja mwaka 2008 na miaka hii ni tofauti?.kama mchezaji anaangalia maslahi yake kwanini klabu isiangalie maslahi ya timu?.Frank lampard ameisaidia sana chelsea kuliko kaseja alivyoisaidia simba lakini lampard akiongezwa mkataba mshahara wake utapunguzwa kutokana na umri wake,Kaseja ni nani mpaka akomae kupewa mshahara mkubwa wakati umri umeenda na kiwango kimeshuka?.Kama Kaseja anaipenda sana simba kwanini aliondoka 2008?.

Hapa tusidanganyane,Kaseja hapendi simba bali alikua anapenda pesa alizokua anapewa simba,pia tupo wengi hatupendi kazi tunazofanya bali tunapenda malipo ya kazi tunazozifanya..Kama viongozi wa simba wamefanya usaliti kwa Kaseja basi Kaseja ndie msaliti wa kwanza.
Hawa ni baadhi ya magwiji wanaokubali mishahara yao ipunguzwe. Je Kaseja ameifanyia nini simba zaidi ya hawa?


Sitashangaa Yesu akimkacha Yuda Iskariote mbinguni,sitashangaa Dortmund wakimtema Sahin kama akishuka kiwango na pia sishangai simba walivyomtema Juma  Kaseja.Kama huu ni usaliti basi Kaseja ndie alikua akihitaji kuisaliti simba,Kaseja kabla ya kutemwa angepata timu ambayo ingemlipa mamilion anayoyahitaji angeondoka Simba,na hicho ndicho alikua anasubiri afanye kama alivyofanya mwaka 2008 ila bahati haikua upande wake viongozi wa Simba wakamuwahi.

...... By Kajage junior

3 comments:

  1. Hata mimi nani kakuambia napenda kazi? Napenda pesa kwenye kazi ndo maana naipenda jumamosi kuliko jumanne.

    ReplyDelete
  2. Hata wewe unapenda chapaa

    ReplyDelete

Powered by Blogger.