SAKATA LA ROONEY: TALAKA SULUHISHO PEKEE LA UHUSIANO HUU

Ukiona ndoa imekua yenye migogoro, hakuna amani, kila mmoja hana imani na mwenzie, suluhu imeshindikana kinachobaki hapo ni Talaka tu..
Rooney akiwa na Sir Alex Ferguson

Hicho ndicho kinachotokea na kuendelea katika ndoa iliyodumu kwa miaka tisa sasa Ndoa kati ya Wayne "Wazza" Rooney na Mabingwa wa England Manchester United kwani ndoa hii imekosa amani na migogoro imekua sehemu ya maisha ya ndoa hii kwa kipindi cha hivi karibuni.

Miaka miwili na nusu iliyopita Wayne Rooney alituma maombi rasmi ya kuomba kuihama Man United huku akihoji malendo ya Timu. Ghafla alibadili maamuzi na kusaini mkataba unaomwingizia Paundi 250,000 kwa wiki.

Kocha aliyestaafu Sir Alex Ferguson hakufurahishwa kabisa na kitendo cha Rooney kuomba kuondoka ila kwa wakati huo hakua na jinsi ilibidi ajishushe na kukaa na Rooney mpaka walipokubaliana na matokeo yake Rooney alisaini mkataba mpya.

Kuwasili kwa Robin Van Persie si tu kuliimalisha safu ya ushambuliaji ya Man United ila kulimpa kiburi Sir. Ferguson cha kukabiliana na Rooney.
Ghafla tukashuhudia Rooney akaanza kuchezeshwa zaidi nafasi ya kiungo, pamoja na kuimudu lakini hafurahii nafasi hiyo.

Ferguson hakuishia hapo aliushangaza ulimwengu baada ya kumwacha Rooney
katika mchezo wa pili wa Ligi ya Mabingwa dhidi ya Real Madrid katika uwanja wa Old Trafford na jinsi msimu wa 2012/2013 ulivyokua ukiendelea alikua akimwanzisha benchi au akipata nafasi ya kucheza hamalizi dakika 90.
Haya yote hayakumfurahisha Rooney ndipo mwishoni mwa msimu ulioisha kabla Sir
Alex Ferguson hajatangaza kustaafu akatuma maombi (japo hayakua rasmi lakini alimwambia Ferguson ) mengine ya kutaka kuondoka.

Ndipo Ferguson akaamua kumuacha katika mchezo wa mwisho wa kocha huyo katika uwanja wa Old Trafford ambapo Ferguson aliagwa rasmi kwa kukabidhiwa kombe la Ubingwa Wa 20 wa England dhidi ya Swansea.

Siku chache baadaye David Moyes akatangazwa kumrithi Ferguson na uvumi wa Rooney kuondoka ukazidi. Hakuna kilichozungumzwa ndani ya United kuhusihana na tetesi hizo ndipo David Moyes akafanya mazungumzo na Rooney kisha kuibuka na kutamka Rooney ni mali ya Manchester United, hivyo hauzwi katika mkutano wake wa kwanza na waandishi wa habari na Mpaka leo Rooney hajasema chochote kuhusiana na kauli ya Moyes.

Akiwa ziarani na Man United Huko Singapore kwa maandalizi ya msimu mpya, ilimlazimu Rooney kurejea nyumbani baada ya kupata maumivu ya misuli paja.Kurejea kwake kulitafsiriwa katika namna mbali mbali lakini wengi wakidhani amerejea Uingereza kukamilisha taratibu za uhamisho.


Ndoa ikazidi kuingia kwenye mgogoro baada ya makamu mwenyekiti wa United Edward Woodward kutamka kuwa Man United haipo tayari kufanya mazungumzo na Rooney  kwa ajili ya mkataba mpya mpaka msimu unaofuata kuisha. Na pia wakiangalia maendeleo yake kiafya na uchezaji.

Kocha David Moyes nae akaibuka na kudai Manchester United si Rooney ila United ni Timu na hayupo tayari kumwona Rooney anakua zaidi ya klabu. Baada ya kauli hiyo
Vyanzo vya karibu na Rooney vikadai amethibisha kua hana furaha na
hafurahishwi na anayotendewa ndani ya Man United.
Wayne Rooney mwenye miaka 27 hayuko tayari kua chaguo la pili mbele ya Robin Van Persie na hayupo tayari kuchezeshwa nafasi ya kiungo ambayo haifurahii..

Lakini pamoja na sakata lote hilo Rooney hajawahi kupeleka Ombi maalumu la kutaka kuondoka Man United kama alivyowahi kufanya Cesc Fabrigas wakati anaondoka Arsenal au Carlos Tevez alipotaka kuondoka Man City.
Haya yote yanathibitisha ni kwa namna gani ndoa hii ipo kwenye mgogoro mkubwa, mpaka kufikia hatua ya Talaka kua suluhisho pekee, huku mabwana wapya Chelsea na Arsenal wakitamani kufunga nae ndoa mpya mkali huyu anayeaminika katika kikosi cha timu ya Taifa ya England.

Imeandaliwa na Abel Chimwejo wa group ya Wapenda Soka (kandanda)
Usisahau ku like page ya Wapenda Soka - Kandanda katika Facebook.

3 comments:

  1. WELL kwa wataalam wenyewe au wale wazee wenyewe hupenda kuwaita wazee wa busara husema kuwa ndoa kama hii ndio ndoa mana ndoa bila misuko suko haiwi so hii ndo inaonekana kuwa ndoa imara na hiki ni kipindi cha misuko suko kikipita mambo yakaua poa na rooney atakuwa moto wa kuotea mbali

    ReplyDelete
  2. wkt rvp anatua united, nilisema hatotamba kwa sababu United imeundwa kupitia Rooney. Nilisema ili Rvp ashine ni lazima rooney atolewe kafara, kitu ambacho sikudhani ni rahisi.
    Lakini ndivyo ilivyotokea. ROONEY ametolewa kafara kwa ujinga wake mwenyewe.
    Naanza kuamini SAF alimsajili RVP ili kumwondoa Rooney kwenye roho ya united.

    ReplyDelete
  3. Hata kama Rooney atabaki itamwia ngumu sana kucheza katika form ile tuliyoizoea so hata mi naunga mkono aende tu ~ Edo

    ReplyDelete

Powered by Blogger.