HABARI 10 KALI ZA SOKA DUNIANI LEO
Msimu mpya wa ligi mbalimbali unakaribia kuanza na Kila kukicha habari tofauti zinatoka kuhusu na maandalizi ya msimu mpya pamoja na tetesi za usajili.
Tutakua tukiwaletea kila siku habari 10 kali zilizotokea katika ulimwengu wa kandanda.
Tukutane mara nyingine.
~~ Edo ~`
Tutakua tukiwaletea kila siku habari 10 kali zilizotokea katika ulimwengu wa kandanda.
- Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania linaendelea kuchunguza kutoroka na kutimkia nje ya Nchi kiungo wa Simba na Timu ya Taifa Mwinyi Kazimoto ambaye alitimka mara baada ya kuisha kwa pambano kati ya Stars na Uganda ambapo Stars walifungwa 1-0. Tetesi zinasema Kazimoto katimkia Uarabuni kujaribu kucheza soka la kulipwa.
Mwinyi Kazimoto |
- Kocha wa Liverpool Brendan Rodgers amefurahishwa na hatua ya kiungo wa Timu hiyo Steven Gerard kuongeza mkataba wa kuendelea kuchezea timu hiyo kwa miaka miwili zaidi.
Gerard
- Baada ya kumkosa Thiago Alcantara,Mabingwa wa England klabu ya Manchester United imemgeukia Kiungo mwingine wa Barcelona Cesc Fabrigas na taarifa zilieleza kuwa United wamepeleka Paundi milion 30 kumnasa Cesc ambaye pia alikua akiichezea Arsenal. Cesc aliwahi kukaririwa akisema anaweza kucheza katika timu mbili tu Barcelona au Arsenal hivyo tusubiri kuona nini kitatokea.
- Winga wa Chelsea Eden Hazard amesema atafurahi kumkaribisha Wayne Rooney wa Manchester United katika kikosi cha Chelsea kama dili la kumnasa mshambuliaji huyo ambaye Kocha Jose Mourinho anadai anamzimia litakamilika huku Ripoti zikieleza kuna asilimia nyingi Wayne Rooney ataondoka Man United msimu huu.
- Manchester City wamekubali ada ya uhamisho paundi milion 27 kumnasa Stevan Jovetic kutoka Fiorentina ya Italia na dili hilo linaweza kukamilika muda wowote ndani ya wiki hii.
- Mabingwa wa Ufaransa Paris Saint German (PSG) leo wamethibitisha Rasmi kumsajili mshambuliaji Raia wa Uruguay, Edison Cavani toka klabu ya Napoli ya Italia kwa ada ya uhamisho paundi milion 55 na kusaini mkataba wa miaka mitano na kuifanya klabu hiyo kuwa na washambuliaji ghali wawili mwingine akiwa ni Zlatan Ibrahimovich.
- Sergio Busquets amesaini mkataba mpya wa kuitumikia klabu yake ya Barcelona, Mkataba utakaomweka Nou Camp mpaka mwaka 2018. Wakati huo huo klabu hiyo imeendelea kumwinda beki wa PSG Thiago Silva ili kumsajili.
- Kocha wa Manchester United David Moyes amemtaka winga wa timu hiyo Luis Nani kubaki klabuni hapo kwani anaamini kuwa Manchester United wanathamini mchango wako na kumuahidi kumpa nafasi ya kucheza zaidi katika kikosi cha kwanza.
- Real Madrid Imeanza mazoezi ya kujiandaa na msimu mpya wa ligi kuu Hispania ambapo wakali wote walikuwepo mazoezini akiwemo Cristiano Ronaldo huku wakiwa chini ya kocha Carlo Ancellot na kocha msaidizi Zenedine Zidane.
- Ushahidi kama Totenham Hotspurs hawako tayari kumuuza Gareth Bale umejidhihirisha baada ya mchezaji huyo kutokea katika kava ya mchezo wa televisheni akiwa amevalia jezi mpya za Spurs huku akiwa na Mkali wa Dunia Lionel Messi. Kukubali kwa mchezaji huyo kutoka katika kava hilo kumetafsiriwa kuwa hana mpango wa kuihama klabu hiyo ya London katika msimu huu.
Tukutane mara nyingine.
~~ Edo ~`
habari zimejitosheleza kazi nzuri kaka
ReplyDeletethanx Venance tutajitahidi kuzileta habari kadri tunavyozipata kutoka katika vyanzo vya uhakika na sio udaku
Delete~Edo~