KOMBE LA DUNIA 2022 KUFANYIKA KATIKA VIWANJA VYENYE AC AU WAKATI WA BARIDI?


Viwanja vitakavyotumika 2022
Hili ni swali ambalo limegonga vichwa vya wadau wengi wa soka kuanzia lilipotamkwa jambo hilo na Rais wa FIFA Sep Blatter ambaye amesisitiza kuwa ataishauri kamati kuu ya FIFA kuhamishia michezo hiyo ya kombe la Dunia mwaka 2022 ambazo kwa mara ya kwanza zitafanyika katika nchi iliyotawaliwa na jangwa kwa asilimia kubwa  Qatar huko Bara Asia ambapo joto ni kama utamaduni wa nchi hiyo.

Kawaida fainali za kombe la Dunia hufanyika kati ya mwezi wa sita na wa saba kila baada ya miaka minne ambapo kwa kipindi hicho nchi nyingi hali ya hewa huwa ya kawaida lakini kwa Qatar hali ni Tofauti kwani mwezi wa sita mpaka mwezi wa saba ni miaezi ambayo joto hupanda na kufikia kati aya nyuzi joto 40-50 kiwango ambacho ni kikubwa sana kwa mwnadamu kuhimili.

Miezi yenye nafuu kwa nchi hiyo ni kuanzia Novemba mpaka Januari ambapo joto hushuka mpaka nyuzi joto 20 hali ambayo ni kawaida kwa nchi nyingi raia wake kuweza kuhimili. Ikumbukwe nchi 32 zinatarajia kuwepo Qatar katika mashindano hayo.

Kamati ya maandalizi ya michuano hiyo ikiongozwa na mwenyekiti wake Hassan Al-Thawadi walishatoa mchanganuo wao na serikali ya Qatar iko tayari kujenga viwanja vya kutumia Air Condition kama michuano hiyo itafanyika miezi ya sita na saba kama ilivyopangwa lakini Blatter amelikataa wazo hilo na kusema "kombe la Dunia ni zaidi ya Mpira uwanjani, ndio wanaweza kuweka Air Condition viwanjani lakini huko mtaani hali itakuaje kwa wageni? Ni hakika hawawezi kuweka Air Condition Nchi nzima"

Kumekua na taarifa tofauti za kupinga jambo hilo kutoka mabosi wa ligi za Ulaya kwa kudai kama mpango huo utapitishwa basi utaathiri ligi zao kwani mwezi wa kumi na moja na kumi na mbili ligi zinakua katikati.

Hivyo kama wadau bado tunasubiri kuona nini kitatokea AC viwanjani au mwezi wa Kumi na mbili?

......Edo ( facebook/ wapenda soka (kandanda) group )

No comments

Powered by Blogger.