KOMBE LA EMIRATES ~ WENYEJI ARSENAL,NAPOLI,FC PORTO NA GALATASARAY UWANJANI.



Kombe la Emirates ambalo huandaliwa na klabu ya Arsenal ya England limerudi tena baada ya mwaka jana kutochezwa kutokana na Michezo ya Olimpiki iliyokua ikifanyika katika jiji la London.

Mashindano ya mwaka huu yatazishuhudia timu nne zikishiriki wenyeji Arsenal, Mabingwa wa Ureno FC Porto, Napoli ya Italia na Mabingwa wa Uturuki klabu ya Galatasaray huku mechi zikichezwa kwa siku mbili yani Jumamosi ya Agost 3 na Jumapili ya Agost 4.

Kama ilivyokua kwa mashindano yaliyopita mashindano ya mwaka huu yatawapa nafasi mashabiki kucheki mechi mbili kwa kiingilio kimoja kwani mechi zitachezwa katika uwanja mmoja tu wa Emirates ambapo mechi ya kwanza itaanza saa 10 jioni siku ya Jumamosi ya Agost 3 ambapo Mchezaji wa zamani wa Arsenal Emmanuel Eboue ataiongoza Galatasaray kuivaa FC Porto ya Ureno kabla ya Arsenal kuwakaribisha Napoli ya Italia siku hiyo hiyo saa 12:20 jioni.

Jumapili ya Agosti 4 Itazishuhudia mechi mbili tena muda huo huo ikitanguliwa na ile ya Napoli na Fc Porto badaye Arsenal watacheza na Galatasaray.

BINGWA WA KOMBE LA EMIRATES ATAPATIKANAJE?

Timu itakayoshinda itajikusanyia pointi 3 na kila droo itahesabiwa pointi moja.
 Kila timu itapata point moja kwa kila goli watakalofunga.
Kama timu zitafungana pointi na magoli basi Wataangalia tofauti ya mashuti yaliyopigwa kulenga goli (shots on Target)
Hivyo basi timu itakayokua na Point nyingi ndiyo itajishindia kombe hilo na kukabidhiwa kombe baada ya mechi ya mwisho ya siku ya Pili ambayo ni Agosti 4.

Je unadhani timu gani itaibuka Kidedea na kubeba kombe hili la Emirates?

.... By Edo Daniel Chibo ( Wapenda Soka(kandanda) group  na Wapenda Soka - kandanda page on facebook )

No comments

Powered by Blogger.